Featured

    Featured Posts

MWENYEKITI CCM WILAYA KIBAHA MJINI AWATAKA VIONGOZI WA MASHINA KUJIAMINI








Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Wilaya ya Kibaha Mjini, Mwl. Mwajuma Nyamka amewataka viongozi wa mashina kufanya kazi kwa kujiamini.


 “Ninyi ni viongozi, jiaminini kwamba mnayo mamlaka kama inavyoeleza katiba ya chama chetu, msijione wadogo au wanyonge,” alisema Mwl Nyamka kwenye ziara ya kutembelea viongozi wa mashina katika Kata ya Mbwawa na Visiga wilayani humo.


 Mwenyekiti huyo kwa kushirikiana na wajumbe wa kamati ya siasa wilaya hiyo wanaendelea na ziara leo katika kata za Viziwaziwa na Kongowe, azma ikiwa ni kutembea katika kata zote kuzungumza na viongozi wa mashina na wengineo katika wilaya nzima.


 “Uchaguzi umekwisha, tuendelee kuchapa kazi,” alisema Mwl. Nyamka.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana