*ASEMA KAMA KIONGOZI WA SERIKALI ANAUONA UHAI WA KANISA HALISI KUDUMU
![]() |
| Rais Samia Suluhu Hassan akiwa kazini |
Na Bashir Nkoromo, Mlimani City
Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi la Mungu Baba ndani na Nje ya Tanzania Baba Halisi amesema kufuatia Tanzania kuwa Chanzo cha Baraka Rais wa nchi Dk. Samia Suluhu Hassan anatakiwa kuinuliwa mikono ili Taifa liendelee kushinda 'vita'.
Wakati Baba Halisi akisema hivyo Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ametamka bila kumung'unya maneno kuwa mahubiri ya Baba Halisi yanayohimiza amani, upendo usiobagua na kila mmoja kuzalisha kwa haki na kusisitiza kila mtu kuamka alfajiri kuwainua watu wote hasa waliopo madarakani ni 'vision' ambayo Mungu mwenyewe anaitaka.
Amesema kwa kuwa Mungu ameshampa Baba Halisi Vision hiyo kazi iliyopo kwa kila mtu ni kumsikiliza kiongozi huyo na kwenda kuiishi vision hiyo, na kwamba kwa msimamo wa Kanisa Halisi wa kutofungamana na siasa na badala yake kuwa na msimamo wa kutaka kila mtu ajue aliyeumba, yeye (RC Chalamila) kama kiongozi wa serikali anauona uhai wa Kansa hilo kudumu.
Kauli hizo 'zimepasua anga' katika Mkutano wa kipekee wa habari njema ulioandaliwa na Kanisa hilo lenye Kao lake Kuu Kiwanja Namba 195, Tegeta Namanga Jijini Dar es Salaam, na kufanyika kwa kishindo katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam, Jumapili, Septemba 10, 2023, sawa na Lango la 26 Eluli 1 Majira Halisi kwa Kalenda ya Kanisa Halisi.
Mkutano huo uliohudhuriwa na maelfu ya Uzao (waumini) kutoka ndani na nje ya Tanzania na waalikwa mbalimbali wakiwemo viongozi wa taasisi za Serikali, Vyombo vya Elimu ya Juu, Vyama vya Siasa, Dini/Madhehebu, Wazee na mkoa wa Dar es Salaam wakiwakilisha jamii, ulilenga kuwajulisha Watanzania kuwa 'Tanzania ndicho Chanzo cha Baraka kwa Mataifa yote', hivyo waishi vipi.
Baba Halisi, aliwaelekeza Watanzania kumuinua mikono juu muda wote ili taifa liendelee kushinda 'vita' alipokuwa akiachilia mada katika mkutano huo iliyohusu 'Kwa nini Tanzania ndicho chanzo cha Baraka kwa mataifa yote',
Ukumbi ukiwa umegubikwa na mandhari ya amani kwa kupambwa kwa vitu vyeupe hadi taa zote kila kona, Mkutano huo ulianza rasmi saa 8 mchana kwa Baba Halisi kuongoza shukurani ya kuubariki mkutano huo, kumuinua (kumuombea) Rais Dk. Samia na viongozi walio chini yake kuanzia juu hadi chini na watu wote.
Baba Halisi akiwa amekamilisha kuongoza shukurani, saa 9 alasiri Mgeni rasmi, RC Chalamila aliwasili na kuufanya ukumbi kulipuka kwa Uzao kucheza kwa furaha mdundo wa wimbo wa kumpokea uliokuwa ukiporomoshwa na Bendi ya Kanisa Halisi ambayo ilikuwa ukumbini tangu saa 6 mchana ikipiga nyimbo za amsha amsha kwa mtindo wa bandika bandua.
"Baraka imeshafika, tunayo furaha tele kukukaribisha ndugu mgeni rasmi, Mheshimiwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, nikuambie tu kwamba, muda siyo mrefu kabla hujafika hapa tumeshamuinua Mheshimiwa rais na wewe pia tumeshakuinua na viongozi wengine kama wewe.
Maana huwa tunaambiwa kila tunapofanya kusanyiko kama hili kabla hatujafanya chochote ni lazima kuwainua viongozi na tumefanya hivyo. Sasa naomba nikueleze, Sisi ni Kanisa Halisi, Kanisa siyo jengo lenya alama ya msalaba bali ni moyo wa yule aliyempokea Muumba, tumeanzia hapa Tanzania.
Tunafundisha mambo makubwa matatu. Kama tunavyovaa vazi hili (jeupe), tuunafundisha amani kwa watu wote, yaani ukikutana na yeyote uwe na amani naye bila kujali itikadi yake wala dhehebu au kabila yake au rangi yake, upendo usiobagua yeyote, na tunasisitiza kuzalisha kwa haki, yaani kila unachokizalisha ukizalishe kwa haki. sasa hayo matatu ndiyo yanayosababisha kila lango (siku) tuamke alfajiri kuinua watu wote na hasa ninyi mlioko madarakani", Baba Halisi akamweleza RC Chalamila.
"Lakini pia Ndugu Mgeni rasmi Kabla hujaja kutukaribisha, natamani ujue kwamba huwa tuna msimamo, msimamo wetu ni kwamba hatujihusishi na siasa. Tukikukuta unaseng'enya viongozi hatuchangii ila umetupa kazi ya kukumbea na kumuombe huyo uliyekuwa unamseng'enya.
Maana katika Yeremia 5:1, kitabu kinasema, "Nendeni Dar es Salaam (akimaanisha mji wowote), mnitafutie angalau mmoja tu anayetamani kutenda kwa haki, ukimpata nitasamehe mji mzima, na katika Mambo ya Nyakati wapili 7:14 hadi 16, kitabu kinasema, "Ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu watanyenyekea na kuacha mambo yao mabaya basi nitasikia maombi yao na jicho langu litakuwa linawatanzama na kuponya nchi yao", Sasa hilo ndilo linatupa kunyenyeke na kumuombea kiongozi kwa hiyo ndiyo msimamo wetu.
Ila pia tuna mtanzamo. Mtazamo tulio nao siyo hizi kuta nne hapana, mtizamo tulio nao tunatamani kila mmoja amjue aliyemuumba. maana ukitaka wote wawe kwenye kuta nne huna pa kuwaweka, utajengaje jengo linatoka hapa hadi Amerika, hutaweza.
Kwa hiyo hatuhudumii hao tu waliopo mbele yangu, hapana tunahudumia mpaka majirani. na katika matoleo tuliyonayo, kapu mojawapo ni la jamii, Muumba wetu tunampa asilimia 10 ya mapato yetu na jamii tunaipa asilimia 5, maana kitabu pia kinatuagiza hivyo katika Isaya 58 ukianzia 7 mpaka12, kinasema "swaumu ambayo Mungu anaitamani ni ukiona ambaye yupo uchi umpe vazi, asiye na chakula umpe chakula, ambaye hajaenda shule umpeleke shule . hiyo ndiyo swaumu ambayo Muumba anaitamani, ndiyo maana tunafanya kazi na jamii", akasema Baba Halisi kumweleza RC Chalamila.
Kisha Baba Halisi akasema; "Mheshimiwa mgeni rasmi, wote hawa waliopo mbele yako wanatamani kusikia salamu zako ili uwakaribishe wajisikie vizuri, hata hao wanangu kutoka mataifa yanayotuzunguka wanatamani kusikia sauti yako. kwa hiyo naomba nikukaribishe utusalimie, utukaribishe, halafu baada yako ndiyo nitaeleza kilichotuleta".
Baada ya kukaribishwa na Baba Halisi, RC Chalamila kwa uhodari mkubwa alio nao katika kuishika hadhira wakati akizungumza akanza kuzungumza kwa kusalimia akisema, " Heri mliobarikiwa na Mungu Baba", makutano wakaitika wakishangilia "Heriiii". akaendelea; "Nilipofika hapa nikaona wote mmevaa mavazi meupe, nikaona ningejua na mimi ninegekuja na vazi jeupe, lakini japo sikuja na vazi jeupe nimekuja na moyo mweupe". ukumbi ukalipuka kumshangilia.
RC Chalamila akasema, hakika Rais Dk. Samia kuwa kiongozi ni maono ya Muumba, akieleza huyo alikotoka tangu kupendekezwa kwenye vikao vya CCM kuwa Mgombea Mwenza na aliyekuwa Mgombea Urais Dk. John Magufuli (ambaye sasa ni hayati).
"Rais wa awamu ya tano kwa maono yake au maono ya Mungu alimpendekeza mbele ya vikao vya chama rais wa awamu ya sita kuwa msaidizi wake na rais huyu alikwenda naye mpaka nyakati za mwisho hata alipoumwa hakumtengua, hadi mauti yalipomkuta, ndipo katiba ikasema rais atakuwa aliyekuwa makamu wa rais, haya yalikuwa maono ya Mungu mwenyewe, na ndiyo maana kama alivyosema Baba Halisi mna wajibu wa kuliweka taifa hili katika mikono ya Mungu. Ni kweli mapambano tuliyonayo tutasalimika kama taifa hili mtaliweka katika jina la Mungu", akasema RC Chalamila.
Kuhusu vazi jeupe kuwa ishara ya amani, RC Chalamila alisema pamoja na Mungu mwenyewe kuwa amesimama mbele lakini wanadamu wanayo nafasi ya kulitengeneza taifa lao na kuongeza kuwa anashukuru rais kwa hekima yake, akisema katika mambo mengi ambayo yamekuwa yakifanyika kwa uchochezi au kawaida lakini amekuwa akiwahimiza viongozi kuendelea kufanya kazi lakini mumuweke mungu mbele.
Kuhusu mafunisho ya Kanisa Halisi kuhimiza kuzalisha kwa haki, RC Chalamila alimpongeza Baba Halisi lakini akaenda mbali zaidi akisema, kuzalisha kwa haki siyo katika Kanisa Halisi tu, ni pamoja na kuwaombea viongozi vipato vyao vipatikane kwa haki ndiyo taifa litapona, siyo viongozi wafiche hela ya Serikali na kwenye kujijengea wenyewe na familia zao.
"Kwa hiyo Baba Halisi anachokihubiri na kutujengea uwezo, unaiona ni 'vision' ambayo Mungu mwenyewe anaitaka, ni vision njema ambayo ameshampa Baba Halisi, kazi kwetu Watanzania kuisikiliza, kuishika na kwenda kuiishi", akasema RC Chalamila.
Kuhusu upendo usiobagua RC Chalamila akasema na kumuasa Baba Halisi akisema; "Baba Halisi ametufundisha hapa pia kuwa na upendo usiobagua. Hii ni kweli, maana pasipo upendo ukristu wetu hauna maana, kwa hiyo mimi Baba nakushukuru sana kwa vision uliyopewa.
Naomba uelewe tu kwamba ukipewa vision na Mungu huwa inaweza kupata vikwazo vingi sana, na viashiria vya vision uliyopewa na Mungu huwa haiendi 'smooth', huwa inapata vikwao vikwazo. Ukiona kuna dalili hiyo ujue hiyo ndiyo kweli vision aliyokupa Mungu".
Akizungumzia kuhusu Kanisa Halisi kutojihusisha na siasa, RC Chalamila alitoa mfano wa Yesu akisema alipozaliwa wana wa Israel walifurahi wakiamini wamepata mkombozi, walihisi atatengua hata baadhi ya mambo yaliyokuwepo katika Falme Israel iliyokuwa chini ya Roma, lakini walipomuuliza kama wataendelea kutawaliwa na kutumia shilingi wanayotumia akawajibu kwamba ya Kaizari wampe kaizari na ya Mungu wampe Mungu.
"Hapo maana yake Kanisa Halisi la Mungu Baba linasema sisi kazi yetu nikuwapa watu ya Mungu siyo ya Kaizari, kwa msimamo huu, mimi kwangu kama kiongozi wa serikali, nauona uhai wa kudumu wa Kanisa Halisi", akasema RC Chalamila na kushangiliwa na makutano ukumbini.
RC akizungumzia kuhusu Kanisa Halisi kukataza kulalamikia viongozi badala yake kuwaombea alitoa mfano wa kwenye sekta ya elimu, akisema, Wakati Rais mstaafu Jakaya Kikwete akiwa madarakani alianzisha mkakati wa ujenzi wa shule za sekondari watu wakalaumu kwamba shule hizo zikiwa kila kona walimu watakuwa hakuna zitakua vilabu vya pombe.
Lakini Dk. Kikwete akaanzisha 'crash program' kwa wahitimu wa kidato cha sita ili wafundishe shule hizo, pia watu wakalalamika kwamba itakuwaje wanafunzi wa sekondari wafundishwe na walimu wa crash program, na pia katika awamu ya tano akisaidiwa na Rais wa awamu ya sita (makamu wa Rais wakati huo), wakasema elimu msingi hadi kidato cha nne iwe bila malipo, na katika awamu ya sita Rais akasema hadi kidato cha sita pia iwe bure.
RC Chalamila akasema, Rais wa awamu ya sita hakuishia hapo alipoona wanyonge ni wengi akaamua kuongeza mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu, na kwamba hatua hizo tangu awamu ya Nne hadi ya sita kuboresha elimu wahitimu wa vyuo vikuu wamekuwa wengi na sasa yamekuja malalamiko kwamba hakuna ajira.
"Sasa kuna wanaofanyabiashara pale Kariakoo wengi ni wahitimu wa darasa la saba na wanatengeneza mamilioni ya fedha, mimi na wenzangu tuliohimu vyuo vikuu tunalalamika hakuna hajira, sasa najiuliza hii mitaala iliyowezesha wahitimu wa darasa la saba kutengeneza amamilioni ni ipi na ile ya vyuo vikuu wanaolalamika hakuna ajira ni ipi? akasema RC Chalamila.
Akasema, kulalamika hakusaidii, kinachotakiwa ni kumtumainia Mungu na kuongeza jitihada za kujituma ili kufikia malengo, Mungu atafungua njia.
Baada ya RC Chalamila kumaliza hotuba yake, Baba Halisi akachukua nafasi kutoa mada ya mkutano huo, lakini kabla ya kueleza akashangaa kukuta RC Chalamila ameshaichambua mada yake kwa sehemu kubwa! Akasema; "kuna jambo limenshangaza, pale pale ninapotaka kusoma ndipo aliposema, yaani pale ndipo kuna bezi ya ujumbe amesoma hapohapo. Nilitaka kuhitimisha kuhusu kulaumiana na yeye amesema hichohicho. Mungu akubariki sana Mheshimiwa mgeni rasmi".
Lakini kama ambavyo husemwa kwamba 'Jungu kuu halikosi ukoko', licha ya RC Chalamila kupita katika njia ileile aliyopanga kupita Baba Halisi, Baba Halisi aliweza kuelea mada yake kwa umahiri mkubwa na kuufanya ukumbi kumshangilia muda wote.
Akitoa Mada yake kuhusu 'Kwa nini Tanzania ndicho chanzo cha baraka kwa Mataifa yote, Baba Halisi alichambua kwa kina mada hiyo ikiwemo kueleza jinsi Tanzania ilivyo kusudi la Mungu Baba tangu Chanzo, akiwataka Watanzania wasitazame shida zinazowafika kwa sababu shida hizo siyo kusudi la Muumba bali kusudi lake kwao ni kuwa matajiri.
Alifafanua kuwa kila mtu amezaliwa ni tajiri lakini wazazi ndio wameingizia watoto mawazo ya kimasikini vichwani na kufuta kusudi kwa kuwaambia mambo ya kimasikini kama kumkataza mtoto asikalie kocho zuri kuwa ni la wageni, asitumie chombo kizuri kula chakula kwamba ni cha wageni.
"Wewe ukilala njaa usilalamike bali angalia kuwa hukukusudiwa ulale njaa, ulikusudiwa uwe tajiri. hata mtoto alizaliwa tajiri ila wazazi ndiyo wanamtia umasikini na kuondoa kilichokusudiwa.
unaposikiliza, sikiliza kilichokusudiwa, unapokaa usisikilize imani sikiliza upendo, imani inatugawa, unaposikiliza usitumie kanuni ya imani tumia upendo. pia usitumie yanayoonekana kwa macho tumia moyo", Baba Halisi akasema..
Baba Halisi akasisitiza kuwa "Nataka ujue ni kweli Tanzania ni Chanzo cha baraka. kwa sababu kuna Sauti kuu nne zilizikika Tanzania. Taifa la kwanza kuitwa Chanzo cha baraka lilikuwa na Sauti ya Musa, Eliya Mtishbi na Yesu, likaitwa Chanzo cha baraka. sasa hapa sauti imesikika mara nne, kwa sababu ya muda siwezi kusema zaidi lakini tafuta hiki kitabu", Baba Halisi akasema huku akiwaonyesha makutano kitabu alichoandika cha 'Kwa nini Tanzania ndicho chanzo cha Baraka'.
Baada ya kueleza kwa kina jinsi Tanzania ilivyo chanzo cha Baraka kwa mataifa yote, Baba Halisi akauliza'
Sasa tunaishije kwenye taifa ambalo limeteuliwa na Muumba kuwa Chanzo cha baraka, kisha akaeleza inavypaswa kuishi.
Akasema; "Kipindi cha Israel iliyokuwa kwanza ndiyo Chanzo cha baraka. Musa akiwa kiongozi wao wakiwa wanatoka Misri kwenda Kaanan, walifika mahali akiwa kiongozi wao, wakawa jeshi la Israel likiongizwa na Joshua wakapigana na jeshi linaitwa Ameriki.
Ukisoma kutoka 17: 11, ili jeshi lishinde vita ilitakiwa mikono ya Musa iwe juu kuanzia asubuhi hadi jioni, akionyoosha jeshi la Israel wanashinda vita, lakini Waisrael walipoanza kumlaumu Musa akawa anachoka mikono inadondoka, wakawa wanapigwa, Hud na Harun akaona wameweke Mussa kwenye kiti, alipoketi wakamshika mikono asubuhi hadi jioni ikiwa juu, jeshi lao likawa linashinda".
Baba Halisi akasema, baada ya Israel sasa ni zamu ya tanzania, akasema; "Tumekuwa Chanzo cha baraka na sisi tuna rais, tuna kiongozi tumemuweka wenyewe kwenye kiti, je, tunamshika mikono mwili au tunamlaumu tu.
Zamu ya Waisrael imetimia ni zamu ya hapa , wao walipomlaumu kiongzi walipigwa, walipomshika mikono wakapiga maadui, je tunamshika mikono?"
"Naomba mkutano mnielewe, hapa sipo katika kuhubiri siasa, nazungumza habari ya Chanzo cha baraka, naomba mjue, yeyote akikaa kwenye kiti cha kuongoza nchi siyio Nafsi, siyo Roho, anakuwa Moyo na ni Moyo wa kila mtu katika hilo taifa, sasa ujue ukimlaumu umelaumu moyo wako, ukimpiga mtama umepiga moyo wako", akasema Baba Halisi.
Baba Halisi akasema, "ujumbe ni kwamba taifa lolote ambalo ni Chanzo cha baraka maisha yake lazima yawe tofauti, yaani wanaishi kwa kuheshimiana, wale mnaofahamu mambo, mnaelewa Israel hawana Katiba kwa sababu ni familia, kwa kuwa wanajijua walikuwa ni Chanzo cha baraka. Nimepona kwa sababu limelisema hili, maana ningedaiwa na Muumba kama nalijua halafu sijasema, nimefurahi na Wazee wa Dar es Salaam wapo hapa", alisema Baba Halisi.
"Mkishakuwa taifa Chanzo cha baraka siyo kwa ajili yenu bali kwa ajili ya wengine. sasa mpo tayari tuiishie njiani kama wale waliosihia njiani? maana wale wa Mussa walipoanza kumlaumu walijiponza wao wenyewe na Mussa pia walimponza, hata ungekuwa na nguvu kiasi gani wakishaanza kukulaumu unaishiwa nguvu".
Kwamba Sauti imeshukua hapa Tanzania ni kweli wala siyo uongo, na kitabu kipo, swali je? tunapokea kuishi maisha ya wale ambao ni Chanzo cha baraka?, Baba Halisi akasema na kuuliza, Kisha akafafanua akisema; "maisha ya aina hii wahawalaumiani, tunatakiwa tuwe na mfumo wa kuongea kifamilia, siyo kutukanana, siyo kutupiana mawe wala kupigana mitama. Mimi nimetimiza siyo kumaliza. tusimame tushukuru", Baba Halisi akasema kisha akaongoza shukurani ya kupokea ujumbe na kukamilisha mkutano.
Wakati huo huo, Baba Halisi alilazimika kuongoza toba ya shukurani na kutoa matunda, baada ya tukio la mtu mmoja aliyemuita kuwa ni rafiki yake, aitwaye Asbedito Mfugale, alipopanda jukwaani kusema neno, lakini katika kuzungumza 'akajimwambafai' pia kuwa Baba Halisi ni shemeji yake ambaye amemuolea dada yake ambaye kwa sasa ni Mama Halisi.
Baada ya Mfugale kujinadi kuwa ni shemeji yake, Baba Halisi ilibidi acheke sana, halafu akasema yeye siyoshemeji yake kwa kuwa Baada ya kuwa Baba Halisi ameshakuwa Baba wa watu wote akiwemo Mfugale na Mama Halisi siyo Dada yake tena kwa kuwa ni Mama Halisi wa wote akiwmo Mfugale baada ya kuwa Mama Halisi.
Kufuatia hilo Baba Halisi aliwaita ndugu waliofuatana na Mfugale, kwenda jukwaani ili kumuachilia abakie kuwa Baba Halisi tu ili apate kutumikia watu wote bila kuzingatia mahusiano ya kindugu ambayo alisema yatasababisha ubaguzi katika huduma yake.
"Sasa naomba mtamke kuwa mimi siyo shemeji yenu, ila ni Baba Halisi", Baba Halisi akasema, kisha Mgungale akasema, "Mimi naomba nitamke tu kuwa Imekuwa", akimaanisha amekubali.
mataifa mane mkongo akasema
kuna rafiki yangunamekuja anaitwa Asbedito Mfugale mkurugenzi usalama wa ang
Picha kem-kem za Mkutano huo ulivyokuwa, tangu mwanzo hadi mwisho 👇
RC CHALAMILA AKIWASILI👇Moja Halisi akiwaatambulisha Watekeleza Sauti kwa RC Chalamila. Kushoto ni mwanakamati ya Mkutano huo Mtekeleza Sauti Thebeth Halisi.
"Huyu ni Msaidizi wa Baba Halisi, anaitwa Faida Halisi, akasema Moja Halisi wakati akiendelea kutambulisha Waatekeleza sauti kwa RC Chalamila.
RC Chalamila akiongozwa kwenda ukumbini.
RC Chalamila akiingia ukumbini.
Baba Halisi (kushoto) na watu wote wakiwa wamesimama kumlaki ukumbini RC Chalamila.
Mama Halisi akimlaki RC Chalamila.
'Mheshimiwa pita hapo ukaketi", Moja Halisi akimuongoza RC Chalamila.
RC Chalamila akiwa na Moja Halisi baada ya kufika meza Kuu. Kushoto ni Mwenyekiti wa Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam Mohammed Mtulia na DAS wa Ilala Beatrice Mbawala.
RC Chalamila akiwa makini kufuatilia hali ya mkutano huoWaimbaji wakitumbuiza baada ya mgeni rasmi RC Chalamila kuwasili ukumbini.
Baba Halisi akimkaribisha ukumbini RC Chalamila. "tunayo furaha tele kukukaribisha ndugu mgeni rasmi, Mheshimiwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, nikuambie tu kwamba, muda siyo mrefu kabla hujafika hapa tumeshamuinua Mheshimiwa rais na wewe pia tumeshakuinua na viongozi wengine kama wewe", Baba Halisi akamwambia RC Chalamila..
Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam wakisimama baada ya kutambulishwa na Baba Halisi uwepo wao kwenye mkutano huo.
Watekeleza sauti wa Nchi za nje wakisimama baada ya kutambulishwa na Baba Halisi uwepo wao kwenye mkutano huo.
Baba Halisi akiinua shukurani ya kumkaribisha RC Chalamila na kumkaribisha kusalimia na kuwakaribisha makutano kwenye mkutano huo
"Mheshimiwa mgeni rasmi, wote hawa waliopo mbele yako wanatamani kusikia salamu zako ili uwakaribishe wajisikie vizuri, hata hao wanangu kutoka mataifa yanayotuzunguka wanatamani kusikia sauti yako. kwa hiyo naomba nikukaribishe utusalimie, utukaribishe, halafu baada yako ndiyo nitaeleza kilichotuleta". akasema Baba Halisi.
RC Chalamila akisalimia na kuwakaribisha kwenye Mktano huo baada ya kukabirishwa na Baba Halisi.
"Nilipofika hapa nikaona wote mmevaa mavazi meupe, nikaona ningejua na mimi ninegekuja na vazi jeupe, lakini japo sikuja na vazi jeupe nimekuja na moyo mweupe". akasema RC Chalamila, ukumbi ukalipuka kumshangilia.
"Nakushukuru Sana Baba Halisi na Mama Halisi kuhudhuria Mkutano huu", akasema RC Chalamila, Baba Halisi na Mama Halisi nao wakainuka kupokea shukurani.
Watekeleza sauti pia wakasimama kupokea shukurani.
RC Chalamila akaendelea kuzungumza huku Baba Halisi akimsikiliza kwa makini.
"....Hapo maana yake Kanisa Halisi la Mungu Baba linasema sisi kazi yetu nikuwapa watu ya Mungu siyo ya Kaizari, kwa msimamo huu, mimi kwangu kama kiongozi wa serikali, nauona uhai wa kudumu wa Kanisa Halisi", akasema RC Chalamila.
RC Chalamila akipongezwa na Baba Halisi baada ya hotuba yake.
RC Chalamila akipongezwa na Mama Halisi baada ya hotuba yake.
Baba Halisi akaongoza shukurani ya kupokea hotuba ya RC Chalamila.
Kisha Baba Halisi akaanza kuzungumza ili kuwasilisha mada ya mkutano huo.
"kuna jambo limenshangaza, pale pale ninapotaka kusoma ndipo aliposema, yaani pale ndipo kuna bezi ya ujumbe amesoma hapohapo. Nilitaka kuhitimisha kuhusu kulaumiana na yeye amesema hichohicho. Mungu akubariki sana Mheshimiwa mgeni rasmi". akasema Baba Halisi.
Hata hivyo Baba Halisi aliendelea kutoa mada ambayo ilisisimua.
"...kila mtu amezaliwa ni tajiri lakini wazazi ndio wameingizia mawazo ya kimasikini vichwani na kufuta kusudi la Muumba kwa kuwaambia watoto mambo ya kimasikini kama kumkataza mtoto asikalie kocho zuri kuwa ni la wageni, asitumie chombo kizuri kula chakula kwamba ni cha wageni.." akasema Baba Halisi, akitoa mada.
"...Nataka ujue ni kweli Tanzania ni Chanzo cha baraka. kwa sababu kuna Sauti kuu nne zilizikika Tanzania. Taifa la kwanza kuitwa Chanzo cha baraka lilikuwa na Sauti ya Musa, Eliya Mtishbi na Yesu, likaitwa Chanzo cha baraka. sasa hapa sauti imesikika mara nne, kwa sababu ya muda siwezi kusema zaidi lakini tafuta hiki kitabu", Baba Halisi anasema huku akiwaonyesha makutano kitabu alichoandika cha 'Kwa nini Tanzania ndicho chanzo cha Baraka'.Kisha Baba Halisi akasimamisha shukurani
RC Chalamila na meza kuu wakipokea shukurani kutoka kwa Baba Halisi.
Kisha Baba Halisi akawaita baadhi ya washiriki kusema waonavyo.
Sheikh huyu akapata nafasi kuzungumza.
Baada ya kuzungumza Sheikh huyo akamsalimia RC Chalamila.
Halafu akazungumza Mjumbe wa Bara la Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam, kueleza mtazamo wake.
"....Baba Halisi nimemuelewa, ukitaka kuishi maisha mazuri soma kitabu hiki alichoandika. ukikisoma ukiwa na busara ya kutosha utamuelewa", akasema Mjumbe huyo wa Baraza la wazee wa mkoa wa Dar es Salaam.
Kisha naye akamsalimia RC Chalamila.
Mjumbe huyo wa Baraza la Wazee mkoa wa Dar es Salaam, akisindikizwa na Mtekeleza sauti Thebeti Halisi kurejea mezani.
Mtekeleza Sauti kutokaCongo DRC pia akapata nafasi ya kuzungumza kwa niaba ya Watekeleza Sauti wa nchi za nje.
Asbedito Mfugale, akizunumza baada ya kupewa nafasi na Baba Halisi.
Asbedito Mfugale, akizunumza baada ya kupewa nafasi na Baba Halisi.
Baada ya Mfugale kujinadi kuwa ni shemeji yake, Baba Halisi ilibidi acheke sana, halafu akasema yeye siyoshemeji yake kwa kuwa Baada ya kuwa Baba Halisi ameshakuwa Baba wa watu wote akiwemo Mfugale na Mama Halisi siyo Dada yake tena kwa kuwa ni Mama Halisi wa wote akiwmo Mfugale baada ya kuwa Mama Halisi.
Hilo likamfanya RC Chalamila acheke kwa furaha.
Baba Halisi akaaita ndugu waliofuatana na Mfugale, kwenda jukwaani ili kumuachilia abakie kuwa Baba Halisi tu ili apate kutumikia watu wote bila kuzingatia mahusiano ya kindugu ambayo alisema yatasababisha ubaguzi katika huduma yake.
Baada ya Mfugale na wezake kumuachilia Baba Halisi katika 'ushesmeji' huo, akawashukuru.
Mnara Mmoja Halisi akitoa matunda baada ya Baba Halisi na Mama Halisi kufanya hivyo baada ya tukio la kumuachilia Baba Halisi.
Waliohudhuria wakiwa kwenye mkutano huo.
Baba Halisi (kulia) akiwashukuru Uzao na Watekeleza Sauti kwa kufanikisha Mkutano wa Mlimani City, alipokutana nao makao Makuu ya kanisa Halisi, Tegeta Namanga baada ya mkutano wa Mlimani City.
MWISHOOOOO.

Post a Comment