Na Bashir Nkoromo, CCM Blog, Tegeta
Je, umewahi kujua kwamba Tanzania ndicho Chanzo cha Baraka kwa Mataifa yote? Nadhani hukupata kujua hilo, ila nina uhakika unajua kwamba Tanzania ni taifa ambalo Muumba amelijaalia kuwa na rasirimali ambazo nyingine hazipo katika taifa lolote duniani.
Kwamba Tanzanaia imejaliwa rasilimali nyingi hilo sina shaka kwamba unajua, maana viongozi wetu akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan, wamekuwa wakituambia hilo na hata matunda ya kuwa na rasilimali hizo tumekuwa tukiyaona.
Hivi itawezekanaje uwe hujui kwamba Tanzania ndiyo nchi pekee duniani yanakopatikana madini ya Tanzanite, mbali na kuwepo madini mengine kama dhahabu na almasi na vivutio vingi lukuki ambavyo huwafanya wageni kuja kuvishangaa?.
Yaani hivi kweli uwe hujui kwamba nchi yako ya Tanzania, ina ardhi kubwa yenye rutuba, misitu, mbuga za wanyama wa kila aina, bahari, maziwa, mito, milima ukiwemo Kilimanjaro ambao una hali za hewa za mabara yote duniani, visiwa kama Zanzibar na Pemba vyenye manukato ya karafuu na upendo uliopitiliza na Lugha ya Kiswahili ambayo imechipukia Tanzania na kusambaa duniani kote?. Hapana utakuwa unajua.
Hivyo basi, ni kweli Mungu ameijalia Tanzania rasilimali adhimu. Sasa kama ni hivyo, hiyo haiwezi kuwa sababu tosha ya kuifanya Tanzania kuwa Chanzo cha Baraka kwa Mataifa yote?
Naona unatamani kunijibu, subiri kwanza utajibu jibu lenye uhakika baada ya kuhudhuria au kufuatilia kwenye vyombo vya habari Mkutano wa kipekee ulioandaliwa na Kanisa maarufu hapa nchini na nchi za nje, linaloitwa Kanisa Halisi la Mungu Baba.
Mkutano huo utafanyika Jumapili hii, Septemba 10, 2023, sawa na Lango la 26 Eluli 1 Majira Halisi kwa Kalenda inayofuatwa na Kanisa Halisi, utaanza saa 8 mchana hadi za 11 jioni, katika Ukumbi maarufu wa mikutano wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi ndani na nje ya Tanzania anayeitwa Baba Halisi, anasema mada kuu ya mkutano huo itakuwa ni 'Tanzania ndicho Chanzo cha Baraka kwa Mataifa yote', na kwamba siyo wa dini, kundi fulani, siasa wala wa kidiplomasia, ni mkutano wa watu wote Watanzania na wasiokuwa Tanzania, lengo kuu likiwa ni kuujulisha umma bila mzaha kuwa Tanzania ndicho chanzo cha Baraka kwa Mataifa yote.
Akizungumza na Waandishi wa habari waliofika Kao Kuu la Kanisa hilo, jana, Tegetea Namanga jijini Dar es Salaam, Baba Halisi alisema, maadalizi ya mkutano huo yamekamilika. Viti 1,200 vimeshalipiwa katika Ukumbi huo wa Mlimani City, na mialiko tayari imeshawafikia watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa nyanja zote, Taasisi, wasomi wakiwemo wa falsafa na theolojia.
Amesema, patashika na hekaheka ya mkutano huo itakolezwa na Bendi ya nyimbo za kumuinua Chanzo Halisi (Muumba), ya Kanisa hilo, kwa kuungurumisha muziki kwa mwendo wa 'bandika bandua' kwa saa mbili mfululizo kuanzia saa 6 hadi saa 8 mchana.
Baba Halisi amesema, baada ya burudani hiyo ya muziki, waalikwa wote wataombwa kuketi, kisha atapanda eneo la kuzungumzia kisha ataeleza lengo la mkutano huo na kulitambulisha Kanisa Halisi kwa wasiolijua walijue, na wanaolijua kidogo walijue sana, kisha atamkaribisha Mgeni rasmi kuzungumza.
Amesema, baada ya mgeni rasmi kuhitimisha hotoba yake, ndipo atapanda tena (Baba Halisi), kuipua mada yenyewe kwa marefu na mapana ikiwemo kueleza kwa nini Tanzania Ndicho chanzo cha Baraka kwa Mataifa yote,
"nikishamaliza kutoa mada tutakaribisha waalikwa mbalimbali kuzungumza ili waseme kama tunalowaabia watakuwa wamelipokeaje, kwamba Tanzania kuwa ndicho chanzo cha Baraka kwa Mataifa yote ni hakika au ni jambo la kufikirika?", akasema Baba Halisi.
Akizungumzia Mkutano huo katika Ibada ya Moyo Mmoja (ya Jumapili), Kao Kuu la Kanisa hilo, Tegeta Namanga, Baba Halisi aliwahimiza Uzao (waumini) watakaohudhuria mkutano huo kujiorodhesha majina yao kwa kuwa kila atakayehudhuria mkutano huo atapewa kitambulisha kwa kufaa.
"Baada ya Ibada ya Moyo Mmoja kila uzao na wengine wote wakaoa hudhuria mkutanoni watapewa vitambulisho na moja kwa moja kwenda kupanda gari, magari yote yatakuwa hapo nje, kwa hiyo kila mmoja ahakikishe anaandikwa jina ili aweze kupewa kitambulisho", alisema Baba Halisi.
"Tungependa kila mtu aone na kusikia kitakachosemwa katika mkutano huu, maana ni wa watu wote, lakini mkutano siyo wa hadhara, unafanyika ukumbini, siyo rahisi watu wote kuwepo ukumbini, kwa hiyo ili kila mmoja aweze kuona na kusikia kitakachosemwa mkutano huu utakuwa 'live' Star Tv na kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo Mungu Baba Tv'.
Kwa hiyo waambieni watakakosa nafasi ya kuwa ukumbini nao pia tutakuwa nao, watutazame katika mawasiliano hayo bila kukosa", akasema Baba Halisi.
Kumbuka Blog ya Taifa ya CCM nayo imealikwa kwa hiyo nayo itakuwa inarusha Live mkutano huo kupitia Channel yake ya CCM Blog Tv Online ambao muda mchache kabla ya kuanza kutakusambazia Link, maana hili ni jambo jema.
"Mkutano huu siyo wa Siasa au dipolomasia, ni wa watu wote, pale Mlimani City siku hiyo Lango la 26 Eluli 1 Majira Halisi yaani Jumapili ya Septemba 10, 2023 tutakuwa Live Star Tv, wale watakaokuwa wahapo kwenye mkutano huo nao watatuona na kutusikia", anasema Baba Halisi kwa msiisitizo. Kisha Baba Halisi akawaita Watekeleza Sauti wa mikoa kuorodhesha Uzao wakaoingia kwenye Mkutano huo ili waandaliwe vitambulisho. Watekeleza Sauti wakiwa mbele ya Baba Halisi kutekeleza wito Watekeleza Sauti wakiwa mbele ya Baba Halisi kutekeleza wito. Uzao wakijiandikisha kuhudhuria mkutano huo. "Vipi hapo mmeshajiandikisha? maana tutatoa vitambulisho kwa wote watakao ingia mkutanoni", akisema Baba Halisi alipoamua kupita kwa Uzao (waumini) kuhakikisha kama wameshajisajili kuhudhuria mkutano huo.
"Na nyie hapo? " akauliza Baba Halisi, Wakajibu "tayariiii".
"Na nyie tayari?" Nao wakajibu Ndiyooo".
"Bila shaka na ninyi tayari mmeshajiandikisha, au siyo?" baba halisi akauliza, ao pia wakajibu "tayariii".
Baba Halisi akirejea Utajirishoni (madhabahuni), baada ya kukagua kama Uzao wamejiandikisha kuhudhuria mkutano huo.
Baadhi ya Uzao wakisoma Kitabu cha 'Kwa nini Tanzania Nchi chanzo cha Baraka kwa mataifa yote' baada ya kugawiwa wakati wa Ibada hiyo. π
π
π
============================
Wakati wa mkutano huo Bendi ya kanisa Halisi ya Muziki wa Kumuinua Chanzo Halisi watakuwepo, na kwa Mujibu wa Baba Halisi watapiga muziki bandika bandua kuanzia saa 6 hadi saa 8 mchana siku ya Mkutano huo wa Mlimani City. Baadhi ya wanamuziki hao wakitumbuiza wakati wa Ibada ya Juzi Jumapili. Mwanamuziki mkongwe ambaye aliwahi kuvuma akiwa bendi za Muziki wa kawaida kama Maquiz du Zaire, King Maluu atakuwepo.π
=======================
TAFADHALI TAZAMA IBADA HIYO YA MOYO MMOJA ILIVYOKUWA LIVEπ
Post a Comment