Sept 08, 2023
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania Mkoa Dar es salaam Cde Mwajabu Rajabu Mbwambo Akiwa ameambatana na kamati yake ya utekelezaji Mkoa wa Dar es salaam. Leo Tarehe 08/09/2023 wamefanya ziara ya kukagua Utekelezaji wa ilani ya miradi ndani ya wilaya ya Ubungo katika Kata ya Kwembe na Kata ya Msiga.
Mradi wa shule ya Wasichana katika masomo ya sayansi. umegharimu zaidi ya Bilioni nne (4) kutoka serikali kuu na Zahanati ya Temboni mradi uliyogharimu zaidi ya milion 100 kutokana na mchango wa wananchi, mfuko wa jimbo, fedha kutoka halimashauri ya manispaa na serikali kuu.
Raisi Dr Samia Anatekeleza ilani ya Uchaguzi kwa vitenda kuhakikisha anafikisha huduma za kijamii kwa wananchi.
Baada ya ukaguzi wa ilani Mwenyekiti Ndg Mwajabu Mbwambo amefanya kikao cha ndani na kuwafunda viongozi na watendaji Uwt wa wilaya, Kata 14 na matawi 137 katika wilaya ya ubungo.
Lengo kuu ni kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kulingana na katiba, kanuni na miongozo ya CCM na UWT.
Kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kuyasemea yale yanayotekelezwa na serikali ya awamu ya sita inayongozwa na Raisi Dr Samia Suluhu Hassan, kujipanga na kuwa na mkakati madhubuti wa kuongeza wanachama, kutoa elimu na kutokomeza ukatili wa kijinsia.
Kuhakikisha Jumuiya ya Uwt inabuni miradi mipya na kuendeleza iliyokuwepo ili kujikwamua kiuchumi.
Amewasisitiza kujipanga barabara na maandalizi ya Uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 kuhakikisha mitaa 90 ya wilaya ya ubungo inatimiza dhana ya 50/50, kwa kuwajengea uwezo na kuwashawishi wanawake wenye sifa kuomba nafasi za uongozi.
Katibu wa Uwt Mkoa Cde Sara Mgoli amewakumbusha viongozi na watendaji hao kwenye uhai wa jumuiya kwa kuhakikisha wanafanya vikao vya kikatiba, kuongeza wanachama na kuwa na mahusiano mazuri baina yao na jamii waliopo na kuwa kimbilio la wanawake katika kutatua changamoto na kuwashauri kuzifikasha ngazi husika.
Uwt Imara#
Jeshi la Mama#
Kazi iendelee#




Post a Comment