Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika Mashariki,v Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ametoa ufafanuzi bungeni leo Septemba 8, 2023, kwamba tathmini hufanyika kwanza kujua tija itakayopata Tanzania kabla ya kuamua kupeleka balozi katika nchi husika.
Ameyasema hayo alipokuwa akijibu maswali wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni leo. Bunge limeahirishwa leo hadi Oktoba 30, 2023.
Naibu Waziri Mbarouk akijadiliana jambo na Naibu Waziri mwenza wa wizara hiyo anayehusika na mambo ya Afrika Mashariki, Stephen Byabato.Mbarouk akiwa na aliyekuwa waziri wa wizara hiyo ambaye kwa sasa amehamishiwa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt Stergomena Tax pamoja na Byabato.
Mdau nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Naibu Waziri Mbarouk akitoa ufafanuzi huo...
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI
BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203



Post a Comment