Featured

    Featured Posts

STARS YAFUNZU AFCON, KUTWAA SH.MILIONI 500 ZA RAIS SAMIA

Na Mwandishi Maalum, Algeria
Timu ya Taifa ya Soka ya Tanzania (Taifa Stars) imefuzu kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya kutoka sare ya bila kufungana (0-0) na Algeria katika mchezo wa mwisho kundi F uliochezwa katika Uwanja wa May 19, nchini Algeria.

Stars ikiwa na alama 8 imeungana na Algeria yenye alama 16 katika kundi hilo kushiriki mashindano ya AFCON yatakayofanyika Ivory Coast na kuziacha nje ya mashindano hayo Uganda waliomaliza na alama 7 na Niger waliomaliza na alama 2 huku.

Tanzania imeshiriki mashindano hayo ya AFCON ikiwa ni kwa mara ya tatu, baada ya mwaka 1980 nchini Nigeria na 2019 nchini Misri.

Kufuatia hatua hiyo, Stars amefuzu pia kujipatia tuzo ya sh. milioni 500 ambazo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan,  aliahizi kuituza timu hiyo ikifuzu kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023 nchini Ivory Coast.

"Mtakumbuka wakati wa kujiandaa na mechi ya Uganda kule nyumbani, Rais alitoa ahadi ya kutoa Shilingi milioni 500, timu ikifuzu. Nafurahi kuwaambia kwamba hizo fedha sio tu kwamba zitatolewa, zimekwisha letwa Wizarani kwa ajili yenu”,  alisema Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Saidi Yakubu, wakati
akizungumza na Wachezaji na viongozi wa timu hiyo jana Septemba 7, 2023 nchini Algeria.

Pamoja na kuwaambia habari hiyo njema, Katibu Mkuu aliwapongeza wachezaji na benchi la ufundi kwa kazi kubwa waliyofanya akisema safari ya matokeo hayo haikuwa nyepesi hadi dakika ya mwisho.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana