Featured

    Featured Posts

SIRI YA USHINDI WA YANGA RWANDA HII HAPA

 
 KIUNGO wa kimataifa wa Rwanda ambaye amewahi kukipiga ndani ya timu za Simba na Yanga, Haruna Niyonzima, amesema mbali na mapokezi makubwa ambayo kikosi cha Yanga itayapata itakapotua nchini Rwanda, pia anaamini timu hiyo ina uwezo mkubwa wa kuifunga Al Merrikh.


Septemba 16, mwaka huu, Yanga wanatarajiwa kuvaana na Al Merrikhya Sudan, katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa nchini Rwanda kusaka tiketi ya kufuzu hatua ya makundi.


Kwa vipindi vitatu tofauti, Niyonzima amewahi kuhudumu katika timu za Simba na Yanga, huku akifanikiwa kushinda makombe matano ya Ligi Kuu Bara ndani ya misimu mitatu mfululizo.


Akizungumzia mchezo huo, Niyonzima alisema: “Nafurahi kuona timu yangu ya Yanga inakuja hapa Rwanda kwa ajili ya mchezo wa kimataifa dhidi ya Al Merrikh, napenda kuwaahidi kuwa nitakuwa mstari wa mbele kuongoza mapokezi, lakini pia kuhakikisha Yanga inapata matokeo ya ushindi na kuondoka hapa wakiwa na tabasamu.”


📂Unajiuliza ni wapi utapata habari za Uhakika kabisa Saa 24 kuhusu soka letu? Basi jibu lako ni @sokalabongonews. Follow Sasa @sokalabongonews Kwa Uhakika wa Taarifa za michezo!


🎙️ @sokalabongonews @sokalabongonews 


#SokaLaBongoNews #SokaUpdates #NguvuMoja #DaimaMbeleNyumaMwiko https://instagr.am/p/CxC1TeGKOq7/

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana