Featured

    Featured Posts

CHONGOLO ANG'AKA KUONA SKIMU YA UMWAGILIAJI KUKWAMA KWA MIAKA 16


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Godfrey Chongolo  akikagua Skimu ya Umwagiliaji ya Ugalla katika Kijiji cha Katambike, wilayani Mpanda, ili kuuwekea mpango wa kuukwamua, baada ya mradi huo kukwama tangu 2007. Ndugu Chongolo amefanya ukaguzi wa skimu hiyo iliyogharimu zaidi ya shilingi milioni 800 wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kusikiliza kero za wananchi na kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020-25 katika Halmashauri ya Nsimbo, Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, leo Ijumaa Oktoba 6, 2023.Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi, Idd Kimanta.



Komredi Chongolo akizungumza na wananchi jinsi atakavyoupatia ufumbuzi mkwamo wa  mradi huo. Chongolo amesema kuwa atakwenda kumueleza Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu changamoto hiyo, ambapo pia atakutana na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe,
Wananchi wakisikiliza kwa makini Komredi Chongolo akizungumza nao



 IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana