Featured

    Featured Posts

JUMUIYA KUU YA WABAPTIST TANZANIA YAWASIMAMISHA WATUMISHI KWA UKIUKWAJI WA MAADILI

Na Lydia Lugakila,
Mwanza

Jumuiya Kuu ya Wabaptist Tanzania imefikia maamuzi ya kuwasimamisha nyadhifa zao watumishi hao ambao ni Peter Sangija aliyekuwa Mkurugenzi wa vijana Taifa na mwenzake Fredrick Mahanyu aliyekuwa naibu katibu mkuu Jumuiya Kuu ya Wabaptist Tanzania, yawasimamisha nyadhifa zao watumishi wawili kwa ukiukwaji wa maadili. 

Maamuzi hayo yamekuja kufuatia kikao cha kamati kuu ya Jumuiya Kuu ya Wabaptist Tanzania kilichohusisha wajumbe kutoka kanda tano, yaani Kanda ya Ziwa, Kanda ya Mashariki, Kanda ya Pwani, Kanda ya Magharibi, na Kanda ya nyanda za juu Kusini kilichofanyika katika kanisa la Baptist Nyamanoro Mwanza.

Jumuiya Kuu ya Wabaptist Tanzania imeeleza kuwa watumishi hao walikwenda kinyume na miongozo ya Jumuiya hiyo na kujivika madaraka ya viongozi wao na kuleta sintofahamu baina ya Jumuiya hiyo Serikali hata jamii pia.

Akizungumzia sakata hilo Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa Jumuiya Kuu ya Wabaptist Tanzania, mchungaji Cosmas Kanunu, alisema jumuiya hiyo imefikia maamuzi hayo ili
Kulinda imani ya Jumuiya hiyo.

"Katika Biblia Yesu alikuwa na Wanafunzi 12 lakini ndani ya hao alikuwemo Yuda ambaye alijiunga na makundi mengine ya nje ambayo hayamujui Yesu Kristo hadi kusababisha Yesu kuuwawa hivyo maamuzi hayo ni vyema yamefanyikaq mapema"alisema mchungaji Kanunu.

Kufuatia hatua hiyo kamati kuu hiyo imemteua Mwalimu Nelsoni Penford Madamanya ambaye ni katibu wa Jumuiya Kuu ya Wabaptist Tanzania Kanda ya Ziwa kuwa naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya Kuu ya Wabaptist Tanzania Wakati nafasi ya mkurugenzi wa vijana ikibaki chini ya Mwenyekiti wa vijana taifa.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya Kuu ya Wabaptist Tanzania Barnaba Michael alisema ni vyema kila mtumishi akafanya kazi yake bila kuvuka mipaka ili kuifanya jumuiya hiyo kuonekana ya mfano.

"Tunahitaji watumishi wa Mungu kurudi kwenye mstari ambao tulijiwekea wenyewe tusifanye tofauti na mifumo iliyopo" alisema mchungaji Barnaba.

Naye Makamu Mwenyekiti Jumuiya Kuu ya Wabaptist Tanzania Mchungaji Deus Kayoka alisema hatua hiyo ni fundisho huku akiwahimiza watumishi hao kuondoa hali ya kutafuta kipato kupitia migogoro.

Hata hivyo kwa upande wake Mwenyekiti mstaafu wa Jumuiya Jumuiya Kuu ya Wabaptist Tanzania Nicholaus Nzella alisema ni vyema mawasiliano ya aina yoyote yanapohitajika kufanyika yafanyike kwa njia sahihi ikiwa ni pamoja na kufuata katiba ya mwaka 2009 hivyo maamuzi ya Jumuiya hiyo yaliyofikiwa ni sahihi. waliokwenda kinyume na miongozo ya Jumuiya hiyo na kujivika madaraka ya viongozi wao.

Akizungumzia sakata hilo Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa Jumuiya Kuu ya Wabaptist Tanzania, mchungaji Cosmas Kanunu, alisema jumuiya hiyo imefikia maamuzi hayo ili
Kulinda imani ya Jumuiya hiyo.

"Katika Biblia Yesu alikuwa na Wanafunzi 12 lakini ndani ya hao alikuwemo Yuda ambaye alijiunga na makundi mengine ya nje ambayo hayamujui Yesu Kristo hadi kusababisha Yesu kuuwawa hivyo maamuzi hayo ni vyema yamefanyika mapema"alisema mchungaji Kanunu.

Kufuatia hatua hiyo kamati kuu hiyo imemteua Mwalimu Nelsoni Penford Madamanya ambaye ni katibu wa Jumuiya Kuu ya Wabaptist Tanzania Kanda ya Ziwa kuwa naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya Kuu ya Wabaptist Tanzania Wakati nafasi ya mkurugenzi wa vijana ikibaki chini ya Mwenyekiti wa vijana taifa.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya Kuu ya Wabaptist Tanzania Barnaba Michael alisema ni vyema kila mtumishi akafanya kazi yake bila kuvuka mipaka ili kuifanya jumuiya hiyo kuonekana ya mfano.

"Tunahitaji watumishi wa Mungu kurudi kwenye mstari ambao tulijiwekea wenyewe tusifanye tofauti na mifumo iliyopo" alisema mchungaji Barnaba.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti Jumuiya Kuu ya Wabaptist Tanzania Mchungaji Deus Kayoka alisema hatua hiyo ni fundisho huku akiwahimiza watumishi hao kuondoa hali ya kutafuta kipato kupitia migogoro.

Kwa upande wake Mwenyekiti mstaafu wa Jumuiya Jumuiya Kuu ya Wabaptist Tanzania Nicholaus Nzella alisema ni vyema mawasiliano ya aina yoyote yanapohitajika kufanyika yafanyike kwa njia sahihi ikiwa ni pamoja na kufuata katiba ya mwaka 2009 hivyo maamuzi ya Jumuiya hiyo yaliyofikiwa ni sahihi.

Hata hivyo Jumuiya hiyo imempongeza Rais Samia kwa namna anavyoyajali madhehebu ya dini huku wakiiomba Serikali kuwashughulikia kwa haraka inapotokea kesi au migogoro.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana