Featured

    Featured Posts

KAIMU KAMISHNA AWATAKA MAKAMISHNA WASAIDIZI WAPYA KUILETEA HESHIMA TANAPA

Na Mwandishi Maalum, Arusha.
Kaimu Kamishna wa Uhifadhi kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Juma Kuji amewataka Makamishna Wasaidizi wachapakazi wapya, kufanya kazi kwa bidii mchana na usiku ili kuliletea heshma Jeshi hilo na Nchi kwa ujumla.

Kaimu Kamishna wa (TANAPA) Juma Kuji alisema hayo jana wakati akiwapandisha vyeo Makamishna Wasaidizi Wandamizi wa Jeshi hilo, katika tafrija iliyofanyika Ofisi za Makao Makuu ya Shirika hilo ( TANAPA) Jijini Arusha.

Alisema kuwa angependa kuona maafisa hayo wanafanya kazi kwa bidii na weledi mkubwa na pia kuwa mfano mzuri katika Taifa la Tanzania na mipaka yake kwa ujumla, kwa kufuata taratibu za mfumo wa Jeshi hilo la Uhifadhi.

"Nimewapandisha vyeo, sasa nataka mkafanye kazi kwa bidii na kwa kufuata taratibu zilizopo ndani ya Jeshi hilo"alisema Kuji.

" Nataka pia muwe viongozi waziri katika maeneo mnayoenda kuyasimamia na kuwa mfano Bora kwa askari na maafisa watakaowaongoza"alisema Kuji.

Aidha amewapongeza Makamisha hao Wasaidizi Wandamizi kwa kuwa wavumilivu katika Jeshi hilo na kuonyesha jitihada mbalimbali za kuhakikisha Jeshi lililopo ndani ya (TANAPA)  linaendelea kufanya vizuri ndani na nje ya Tanzania kwa kulinda na kusimamia rasmilimali za Taifa.

Kaimu Kamishna Uhifadhi (TANAPA) alitoa wito kwa maafisa na askari wengine kutoa ushirikiano kwa viongozi wapya waliyovarishwa vyeo ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Kamishna Kuji alifunga tafrija hiyo kwa kuwataka viongozi wote wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) katika kuongeza idadi ya watalii kutoka ndani na nje ya Nchi, ili kusudi waweze kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya Sita inavyotaka.

Kaimu Kamishna wa TANAPA Juma Mussa Kuji, akimvisha cheo John Nyamhanga, kuwa Kamishna Mwandamizi, tukio lililofanyika jana.  (Picha na Cecy Jeremiah).
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana