Featured

    Featured Posts

MILIONI 85 ZAKAMILISHA UJENZI WA KAFANANA YA MATENGENEZO YA VIFAA TIBA IRINGA.




 IRINGA,Octoba 24,2023.

SERIKALI kupitia wizara ya Afya imesema itaendelea kuwajengea uwezo nje ya nchi wataalamu wa Afya ili waweze kuongeza ujuzi wa namna bora ya kutengeneza vifaa tiba vitakavywahudumia wananchi kwa muda mrefu.


Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu wizara ya Afya Dkt.Grace Maghembe wakati akizungumza mkoani Iringa mara baada ya kufungua na kukabidhi karakana ya matengenezo ya vifaa tiba katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.


Karakana hiyo imejengwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Uswis kupitia mradi wa Health Promotion and Systeam [HPSS ] na kugharimu kiasi cha zaidi ya Milioni 85.


Dkt.Grace alieleza kuwa lengo la serikali kuwapeleka wataalamu hao wapatao zaidi ya 30 katika nchi ya Hungali na China ni kuwaongezea ujuzi wa namna ya utengenezaji vifaa viba ili viweze kutoa huduma kwa muda mrefu


 Aliongeza kuwa Serikali imeamua kujenga karakana hizo kila Hospitali kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata huduma zote za Afya kunzia Hospitali ya rufaa, wilaya na Vituo vya Afya nchi nzima.


Awali akitoa taarifa fupi ya ukarabati na uwekaji wa vifaa tiba na samani Meneja mradi wa [HPSS] Ally Kebby alieleza kuwa zaidi ya milioni 85 zimetumika kukamilisha ujenzi wa mradi huo unaotajwa kuwa mwarobaini wa uhaba wa vifaa tiba katika hospitali hiyo.


Kwa upande wake mhandisi wa vifaa tiba katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa Rainfrida Kadinda akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za karakana alisema kuwa kutokana na Serikali kuboresha mazingira ya kazi hivi sasa kutawezeshakufanya kazi kwa ufanisi zaidi ukilinganisha na hapo awali.



‘’Tunaishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wake Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha kwa ajiliya ununuzi wa vifaa tiba na kuboresha huduma za afya hapa nchini’Alisema


MWISHO.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana