Ashrack Miraji Same
Mbunge wa Same jimbo la Mashariki Mhe. Anne Kilango amesema Michezo inasaidia kuwajengea vijana mahusiano mazuri katika nyanja mbalimbali ikiwemo za kielimu pia kuachana na vitendo viovu kama matumizi ya Dawa za kulevya (bhangi na Mirungi).
Ameyasema hayo katika mahojiano na Mwandishi wetu
kuelekea uzinduzi michuano ya Samia Cup inayo tarajiwa kuanza November mosi mwaka huu 2023 katika jimbo la Same Mashariki Mkoani kilimanjaro.
"Dhamila yangu kwa vijana ni kubwa ninacho hitaji ni kuona wanafika mbali na kutimiza Ndoto zao hivyo nitakuwa nao bega kwa bega katika kuleta Maendeleo chanya kwenye Jimbo letu la Same Mashariki".Alisema Mhe. Anne Kilango.
Amesema si mara ya kwanza kuazisha mashindano ya aina hiyo mwaka uliopita wa 2022 aliandaa pia mashindano yliyojulikana kama Kilango Cup, mashindano ya mwaka huu ya Samia Cup ni yanalenga kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kuendeleza vijana kwenye sekta ya Michezo.
"Tumeona Rais akiwekea kipaumbele uhamasishaji wa Michezo Nchini kwetu na kila mmoja anaona matunda yake, tumeona akihamasisha michezo mbalimbali na kutoa motisha za moja kwa moja kwenye vilabu mbalimbali vinvyo shiriki Michezo hata ya kimataifa, na sisi ambao tupo huku moja kwa moja kwa wananchi lazima tushiriki kwa nafasi zetu kuwawezesha vijana nao kupata nafasi ya kushiriki Michezo kwenye maeneo yao". Alisema Mbunge huyo wa Jimbo la Same Mashariki.
"Niseme ukweli wa dhati Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani amenifanyia makubwa katika jimbo langu amenijengea vituo vya afya, barabara , shule nashukuru sana kwa Mchango wake mkubwa hasa kwa Wananchi Wangu wa jimbo la Same Mashariki".
Mwisho.
Post a Comment