Featured

    Featured Posts

PURA: MIONGOZO YA SERIKALI CHINI YA JEMEDALI RAIS DK. SAMIA IMEWEZESHA USTAWI WA SEKTA NDOGO YA MAFUTA NA GESI ASILIA NCHINI

Na Bashir Nkoromo, Official CCM Blog, Dar es Salaam
Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imeishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Jemedali Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa miongozo na maelekezo ambayo yamewezesha ustawi wa sekta ndogo ya mafuta na gesi asilia nchini.

Pia imeishukuru Serikali chini ya Rais Dk. Samia, kwa kuwezesha mazungumzo ya utekelezaji wa mradi wa usindikaji wa gesi asilia kuwa katika hali ya kimiminika (LNG project), mradi ambao taasisi hiyo imesema utaliletea Taifa manufaa makubwa kwa kuanzia fedha, ajira, uanzishwaji wa viwanda vinavyotumia gesi kama malighafi pamoja na uuzaji wa bidhaa mbalimbali.

Akichambua kwa wahariri wa habari andiko kuhusu utendaji na mafanikio ya PURA Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Mhandisi Charles Sangaweni. amesema, chini ya usimamizi na miongozo bora ya Serikali, taasisi hiyo imekuwa imara katika utendaji wake.

Mhandisi Sangawe alichambua andiko hilo katika kikao kazi baina ya Uongozi wa PURA na Wahariri hao wa habari, kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) na kufanyika katika ukumbi wa Zanzibar, uliopo katika Hotel ya Hyatt Regency the Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, leo.

Kwa hakika Mhandisi Sangaweni amezungumza mengi ya utendaji na mafanikio ya PURA, ambayo hata baadhi ya wahariri kadhaa waliohudhuria walikiri kwamba walikuwa hawayajui, hivyo bila kupunguza chochote Blog ya Taifa ya CCM (CCM Blog) inakuwekea andiko lote kama alivyoliwasilisha Mhandishi Sangawe kwenye kikao kazi hicho. Hilo hapo

HOTUBA YA MKURUGENZI MKUU WA PURA WAKATI WA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI AKIELEZEA MAFANIKIO YA UDHIBITI NA USIMAMIZI WA SHUGHULI ZA MKONDO WA JUU WA PETROLI CHINI YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

Ndugu zangu kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina,
Ndugu Viongozi wa Jukwaa la Wahariri
Ndugu Wanahabari,Ndugu Watumishi wenzangu wa PURA,
Ndugu Wanahabari,
Mabibi na Mabwana,


NAWASALIMU KWA JINA LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

Ndugu Wanahabari, 

Awali ya yote napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kufika siku hii ya leo tukiwa na afya njema. Vilevile, nachukua nafasi ya kipekee kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi imara ambao umewezesha Taasisi hii muhimu kutekeleza majukumu yake kwa ufasaha na ufanisi wa hali ya juu.

 

Kwa upande mwingine shukrani zangu ziende kwa viongozi na watumishi wa Wizara ya Nishati, ambayo inaongozwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dotto Biteko, kwa miongozo na maelekezo mbalimbali yaliyowezesha utekelezaji wa majukumu yetu ipasavyo. Aidha napenda kuwashukuru nyinyi ndugu zangu kwa kuweza kufika ili kutusikiliza kwa yale ambayo nitawaeleza juu ya mafanikio ambayo PURA na sekta hii kwa ujumla imeyapata kupitia usimamizi na udhibiti wa shughuli za mkondo wa juu wa petroli.

Ndugu Wanahabari,     
Tangu kuanza kwa shughuli shughuli za utafutaji na uendelezaji wa mafuta na gesi asilia nchini zilianza mwanzoni mwa miaka ya 1950, na kwa kipindi chote hicho Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha shughuli hizi zinafanyika kwa ufanisi mafaniko ili kuwezesha upatikanaji wa rasilimali hii muhimu kwa maendeleo endelevu ya nchi. Kati ya hatua muhimu ambazo Serikali imeendelea kuchukuwa ni kuimarisha mifumo ya Kisheria, Kitaasisi na udhibiti wa shughuli hizo. Hii ili pelekea kuwepo kwa Sheria ya Petroli ya mwaka 1980, Mikataba kifani ya ugawanaji mapato (Model PSA) kwa nyakati mbalimbali, Kanuni na miongozo mbalimbali na Sheria ya Petroli ya mwaka 2015, ambayo kutokana na Sheria hii Taasisi ya PURA ilianzishwa.

Ndugu Wanahabari, 

Kama nilivyoeleza Taasisi ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) ilianzishwa mwaka 2015, kupitia Sheria ya petroli ya mwaka 2015 ambapo ilianza shughuli zake rasmi mwezi Februari 2016 kupitia Kamati Maalumu iliyoundwa na Watumishi kutoka iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini na kutoka TPDC. Kamati hii ilikuwa ikitekeleza majukumu ya Kisheria ya Taasisi huku ikiendelea na maandalizi ya nyaraka mbalimbali za kuwezesha Taasisi kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Ndugu Wanahabari, 

Kwa sasa PURA ina miaka nane (8) na inatekeleza majukumu yake kama yalivyoaisnishwa kwenye Sheria ya Patroli 2015, kifungu cha 12. Majukumu hayo yamegawanyika katika makundi makuu matatu ambayo ni pamoja na Kuishauri Serikali kupitia Waziri mwenye dhamana ya nishati hususani mafuta na gesi juu ya masuala yanayohusu shughuli za mkondo wa juu wa petroli, Kudhibiti na kusimamia shughuli zote za mkondo wa juu wa petrol na kusimamia miradi ya kubadili gesi kuwa katika hali ya kimiminika (Liquified Natural Gas – LNG). Hapo awali shughuli hizi zilikuwa zikitekelezwa na TPDC baada ya kukasimishwa na Kamishna wa Mafuta na Gesi.

Ndugu Wanahabari, 

Shughuli hizi za utafutaji na uendelezaji wa mafuta na gesi nchini zinatekelezwa kwa kupitia mikataba ya ugawanaji mapato yaani Production Sharing Agreements – PSA, ambapo Kampuni kubwa za mafuta duniani huingia mkataba na Serikari na kuwekeza katika nyanja hiyo. Kwa sasa tuna Kampuni zipatazo nane (8) ambapo mikataba iliyopo ni kumi na moja (11); kati ya mikataba hiyo, mitatu ipo katika hatua ya uzalishaji na uendelezaji wa gesi asilia wakati iliyobaki bado ipo katika hatua ya utafutaji.

Ndugu Wanahabari, 

Kama nilivyoeleza hapo awali shughuli za
Historia fupi ya shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi asilia hapa nchini zilianza mwanzoni mwa miaka ya 50 na hadi sasa mafanikio yaliyopatikana ni kama ifuatavyoni pamoja na yafuatayo:

(a) Jumla ya Vvisima vya utafutaji wa mafuta vilivyochimbwa nchini ni 96 ambapo kati ya visima hivyo, visima 59 vipo maeneo ya nchi kavu na visima 37 vipo maeneo ya baharini.

• Gesi asilia imegunduliwa katika visima 44 kati ya visima 96 vilivyochimbwa; 
• Kati ya visima hivyo 44 vilivyogundulika gesi, visima kumi na sita (16) vilichimbwa nchi kavu na ishirini na nane (28) vilichimbwa baharinivya ugunduzi, visima 16 vipo nchi kavu na visima 28 vipo baharini.

(b) Gesi asilia imegunduliwa katika maeneo ya Songo Songo (1974); Mnazi bay (1982), Mkuranga (2007), Kiliwani Kaskazini (2008), Ntorya (2012), Ruvu (2016) na Kina Kirefu cha Bahari (kuanzia miaka ya 2010);.

(c) Gesi asilia iliyogunduliwa nchi kavu na kina kirefu cha bahari ni Futi za Ujazo Trilioni 57.54 (nchi kavu Trilioni 10.41 na Baharini Trilioni 47.13).
    
(c)(d) Uzalishaji wa gesi asilia ulianza mwaka 2004 kwa upande wa Songo Songo na mwaka 2006 kwa upande wa Mnazi Bay.

(d)(e) Ugunduzi huo na uzalishaji wa gesi asilia iliyogunduliwa umewezesha kuanza ikutumikea kwa gesi asilia kama chanzo cha nishatimaeneo mbalimbali, hususan kwa kuzalisha umeme, kutumika viwandani, majumbani na kwenye magari. Hadi sasa kiasi cha gesi kinachozalishwa kinachangia karibu asilimia 70 ya umeme unaozalishwa hapa nchini.

(e) Uzalishaji wa gesi asilia ulianza mwaka 2004 kwa upande wa Songo Songo na mwaka 2006 kwa upande wa Mnazi Bay.

(f) Hadi sasa kwa kupitia usimamizi wa PURA maeneo ambayo yamefanyiwa tafiti ni kiasi cha kilomita za mraba 534,000 ambapo kati ya hizo kilomita za mraba 394,000 ni nchi kavu na km 140,000 baharini, hata hivyo maeneo mengi yameshafanyiwa tafiti za awali ambapo data, taarifa na takwimu zake zipo (Gravity/Magnetic and 2D seismic);

(g) Hadi sasa nchi yetu ina Mikataba ya Utafutaji, Uendelezaji na Uzalishaji Mafuta na Gesi Asilia (PSA) ipatayo 11, kati ya hiyo Mitatu ipo katika hatua ya uzalishaji wakati Mikataba Nane (8) ipo katika hatua mbalimbali za utafutaji.

(h) Kuimarika kwa shughuli za kaguzi za gharama na matumizi katika Mikataba ya PSA.

(i) Kuimarika kwa mifumo ya kisera, kisheria, kikanuni na kitaasisi nchini, ambapo kumekuwa na Sheria ya Peroli ya mwaka 1980, Sera ya Nishati ya mwaka 2015, Sheria ya Petroli ya mwaka 2015, na Sheria ya Udhibiti wa Mapato ya Mafuta na Gesi ya mwaka 2015. Mifumo ambayohii imewezesha kuanzishwa kwa PURA na EWURA.

Ndugu Wanahabari, 

Kwa upande mwingine
kKatika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uUongozi mMahiri wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, PURA katika kutekeleza majukumu yake ya kuishauri Serikali kuhusu masuala ya mkondo wa juu wa petroli, udhibiti na usimamizi wa shughuli hizo imewezesha kupatikana kwa mafanikio yafuatayo:

(a) Kuimarika kwa shughuli za Kaguzi za Gharama katika Mikataba ya Uzalishaji na Ugawanaji Mapato (PSA Audit), iliyopelekea kuokoa fedha kiasi cha zaidi ya Shilingi bilioni 189 kwa kurudishwa kwenye mfuko wa ugawanaji wa mapato kati ya Serikali na Waendeshaji wa Vitalu husika,;

(b) Kuimarika na kuongezeka kwa ushiriki wa Wazawa katika miradi ya utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia nchini. Wastani wa ushiriki wa Wazawa katika shughuli za mkondo wa juu wa petroli kupitia ajira ni asilimia 85,;

(c) Kushauri Serikali na kufanikisha kutolewa kwa ongezwa kwa muda wa leseni ya utafutaji awamu ya pili katika VKitalu vycha Tanga, Ruvu, Mtwara na vitalu Namba 1, 2 na 4 vilivyopo baharini;,

(d) Kushauri Serikali na kufanikisha utiaji saini kwa mkataba wa nyongeza wa uzalishaji na ugawanaji mapato ya gesi iliyogundulika Ntorya katika kitalu cha Ruvuma. Mkataba huo ambao utekelezaji wake utawezesha kuendeleza gesi asilia ya Kitalu hicho ya takriban Futi za Ujazo Trilioni 1.6 ulisainiwa baina ya Wizara ya Nishati, TPDC na Kampuni ya ARA (Oman),

(e) Kushauri Serikali na kufanikisha kutolewa kwa leseni ya utafutaji awamu ya pili katika Kitalu cha Tanga,

(f) Kutoa kibali cha utafutaji wa awali (reconnaissance permit) wa mafuta na gesi asilia katika Kitalu cha Eyasi Wembere kwa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC),

(g) Kuanza kwa kazi uya kufanikisha durusu ya Mkataba Kifani wa Uzalishaji na Ugawanaji wa Mapato (MPSA) kwa lengo la kuhuisha ili kuendana na mazingira ya uwekezaji wa sasa katika sekta ndogo ya mafuta na gesi asilia. Kukamilika kwa mapitio ya MPSA ni hatua muhimu kuelekea zoezi la kunadi Vitalu vya utafutaji wa mafuta na gesi asilia,

(h) Kuongezeka kwa wastani wa uzalishaji wa gesi asilia kufikia Futi za Ujazo Bilioni 53.19 kwa kipindi cha Julai 2022 hadi Februari 2023 ukilinganisha na Futi za Ujazo Bilioni 46.96 kwa kipindi kama hicho kwa mwaka 2021/22, sawa na ongezeko la asilimia 14; na,

(i) Kukamilika kwa maandalizi ya rasimu ya Ramani ya Kidijitali (Interactive Digital Petroleum Reference Map) kwenye Mfumo wa Taarifa wa Kijiografia (Geographical Information System – GIS) inayotoa taarifa za Vitalu vya utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia nchini,

(j) PURA kuweza kuongeza idadi ya watumishi wake ambapo Serikali ilitoa kibali na kufanikiwa kuajiri jumla ya watumishi wapya 22, na

(k) Kuongoza na kushiriki kikamilifu majadiliano ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa uchakataji na usindikaji wa gesi asilia kuwa kimiminika (LNG).

HITIMISHO
Ndugu Wanahabari,
Tangu kupata uhuru Tanzania imepitia changamoto mbalimbali katika eneo la utafutaji wa mafuta na gesi. Changamoto zilizojitokeza zilipatiwa ufumbuzifanyiwa kazi na hatimaye kufikia hatua tuliyopo ambapo kumefanyika ugunduzi wa gesi asilia nyingi ambayo matumizi yake yana manufaa makubwa kwa Taifa na hasa hasa kwenye kuinua uchumi wetu.

Ndugu Wanahabari,
Kipekee kabisa nachukua nafasi hii nikuishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha mazungumzo ya utekelezaji wa mradi wa usindikaji wa gesi asilia kuwa katika hali ya kimiminika (yaani LNG project), mradi ambao utaliletea Taifa manufaa makubwa kwa kuanzia fedha, ajira, uanzishwaji wa viwanda vinavyotumia gesi kama malighafi pamoja na uuzaji wa bidhaa mbalimbali.

Ndugu Wanahabari,
Mwisho nachukua nafasi hii kwa mara nyingine kuniishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa miongozo na maelekezo ambayo yamewezesha ustawi wa sekta ndogo ya mafuta na gesi asilia nchini.  Aidha, naishukuru Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kuratibu mkutano huu pamoja na nyinyi ndugu zangu kwa kufika na kutusikiliza, ni matumaini yangu kuwa mtaendelea kuwa mabalozi wetu katika kuufikishia umma yale mazuri tunayoyatekeleza kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu na manufaa kwa watanzania kwa ujumla.

ASANTENI SANA.

Baada ya wasilisho hilo washiriki walipata nafasi ya kuuliza maswali. kupewa ufafanuzi na pia kushauri.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) Mhandisi Charles Sangaweni.akichambua kwa wahariri wa habari andiko kuhusu utendaji na mafanikio ya PURA, katika kikao kazi baina ya Uongozi wa PURA na Wahariri hao wa habari, kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) na kufanyika katika ukumbi wa Zanzibar, uliopo katika Hotel ya Hyatt Regency the Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, leo. Anayemsikiliza kwa makini ni Salim Said Salim kutoka Chama cha Waandihi wa Habari Tanzania )TEF).Rogasian Mguni kutoka PURA.
 
Washiriki wakimsikiliza Mhandisi Sangaweni.
Washiriki wakimsikiliza Sangaweni.
Washiriki walipokuwa wakisubiri kikao kazi hicho kuanza.
Baadhi ya viongozi kutoka PURA wakiwa kwenye kikao kazi hicho.
Afisa Habari na Mawasiliano kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) Sabato Kosuri akitoa utangulizi na lengo la Kikao kazi mwanzoni.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana