Featured

    Featured Posts

TAASISI ZAIDI ZA HABARI ZAJITOKEZA KUTOA MAONI KAMATI YA TIDO MHANDO

Na Richard Mwaikenda

TAASISI zaidi za habari zimejitokeza kutoa maoni kuhusu tathmini ya hali ya uchumi wa vyombo vya habari na waandishi wa habari katika vikao vinavyoendelea kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO, jijini Dar es Salaam.

Taasisi zilizojitokeza jana Novemba 3, 2023 ni;Taasisi za Baraza la Habari Tanzania (MCT),  Umoja wa Klabu Waandishi  Habari Tanzania (UTPC), Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-Tan), Wakfu wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Shirika la Habari za Maendeleo Tanzania (KADIO) na Chama cha Waandishi wa Habari za Vijijini (RUJAT) pamoja na Angaza Directory iliyoelezea mfusa rahisi wa upatikanaji wa matangazo kwa vyombo vya habari.

Kamati hiyo ambayo iliundwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Technolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye imeanza kupokea maoni hayo wiki hii katika Ofisi za Idara ya Habari zilizopo Mtaa wa Samora, jengo la TTCL ghorofa ta tatu.

Wadau wa habari walioanza kutoa maoni yao mbele ya Kamati hiyo Novemba Mosi, 2023 ni Jumuiya  ya Wanahabari ya Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA), Global Online TV,  Ayo TV na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF).

Kamati itaendelea na kazi ya kupokea maoni siku ya Jumatatu Novemba 6, 2023 ni; Mamlaka ya Mawasiliani Tganzania (TCRA), Idara ya Habari Maelezo, Taasisi za elimu zinazofundisha uandishi wa habari ambazo ni; Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)  SMJC,, SAUT, TUDARCO, MUM OUT na Tumaini University, 

Novemba 7, 2023 itakuwa zamu ya Taasisi  za kimataifa na washirika wa maendeleo , UNESCO, Swiss Development Corporation (SDC), USAID, DW Akademie,  IMS,  BBC Media Action na Internes.

Aidha, Kamati imeanza awamu ya pili ya kusambaza madodoso juu ya suala hilo yanayotakiwa kujazwa na waandishi wa habari pamoja na wafanyakazi walio kwenye vyombo vya habari.


Kamati iliyopewa jukumu hilo ina wajumbe wafuatao: Tido Mhando (Mwenyekiti), Dkt. Rose Reuben (Makamu Mwenyekiti), Mobhare Matinyi (Katibu), Sebastian Maganga, Richard Mwaikenda, Bakar Machumu, Joyce Mhavile, Kenneth Simbaya na Jacqueline Woiso

Baadhi ya wajumbe wa Kamati wakiwa na wadau wa habari kutoka Taasisi mbalimbali za habari waliofika kutoa maoni yao kwenye kamati hiyo.Wajumbe waliopo kwenye picha hiyo ni Richard Mwaikenda (wa nne kutoka kushoto) na Kennerd Simbaya (aliyevaa koti katikati).

Mjumbe wa Kamati Kannerd Simbaya (kushoto) akiongoza kikao hicho.
Mjumbe wa Kamati Jacqueline Woisho (kushoto) akinukuu baadhi ya maoni ya wadau wa habari.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakfu wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Dastan Rafael akitoa maoni kwa niaba ya mfuko huo.



Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Vijijini (RUJAT), Felix Mwakyembe akitoa maoni kwenye kamati hiyo.

Vijana kutoka Taasisi ya Angaza Directory wakielezea jinsi walivyobuni mfumo wa kurahisisha upataikanaji wa biashara ya matangazo kwa vyombo vya habari. Kushoto ni      Dotto Richard na Benard Mwitumba.

 
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana