Featured

    Featured Posts

WAHARIRI WAKONGWE WAJITOKEZA KUTOA MAONI KAMATI YA TIDO MHANDO

 

Na Richard Mwaikenda

Utoaji maoni umepamba moto katika Kamati ya tathmini ya hali ya uchumi wa vyombo vya habari na waandishi wa habari ambapo safari hii idadi ya wadau imezidi kuongezeka miongoni mwao wakiwemo wahariri wa habari wakongwe na waandamizi.

Wengi wa wahariri waliohudhuria kikao kilichofanyika- Novemba 9, 2023 katika ukumbi wa Ruaha katika Kituo cha Mikutano cha  Kimataifa cha Mwalimu Julius  Nyerere jijini Dar es Salaam, ni wanachama wa  Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na wengine kutoka Taasisi zingine za habari.


Baadhi ya wahariri hao wakongwe waliohudhuria kikao hicho na kutoa maoni yao kwenye kikao hicho ni; Joseph Kulangwa, Yasin Sadick, Jesse Kwayu, Muhidini Issa Michuzi, Wallace Maugo, Reginald Miruko, Khadija Kalii na Beatrice Moses.


Baadhi ya wadau waliojitokeza hadi sasa kutoa maoni wanatoka katika  Baraza la Habari Tanzania (MCT),  Umoja wa Klabu Waandishi  Habari Tanzania (UTPC), Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-Tan), Wakfu wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Shirika la Habari za Maendeleo Tanzania (KADIO) na Chama cha Waandishi wa Habari za Vijijini (RUJAT) pamoja na Angaza Directory iliyoelezea mfusa rahisi wa upatikanaji wa matangazo kwa vyombo vya habari.


Novemba 10, 2023 kamati imehitimisha utoaji maoni Novemba 10, 2023 kwa kuwakaribisha wamiliki wa vyombo vya habari.


Kamati hiyo ambayo iliundwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Technolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye ilianza kupokea maoni hayo Novemba Mosi, 2023 katika Ofisi za Idara ya Habari zilizopo Mtaa wa Samora, jengo la TTCL ghorofa ta tatu.

Wadau wa habari walioanza kutoa maoni yao mbele ya Kamati hiyo Novemba Mosi, 2023 walitoka Jumuiya  ya Wanahabari ya Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA), Global Online TV,  Ayo TV na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF).

Kamati iliendelea na kazi ya kupokea maoni siku ya Jumatatu Novemba 6, 2023 kwa wadau waliotoka Mamlaka ya Mawasiliani Tanzania (TCRA), Idara ya Habari Maelezo, Taasisi za elimu zinazofundisha uandishi wa habari ambazo ni; Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)  SMJC,, SAUT, TUDARCO, MUM OUT na Tumaini University, 

Novemba 7, 2023 ilikuwa zamu ya Taasisi  za kimataifa na washirika wa maendeleo , UNESCO, Swiss Development Corporation (SDC), USAID, DW Akademie,  IMS,  BBC Media Action na Internes.

Aidha, Kamati ilisambaza madodoso juu ya suala hilo yaliyotakiwa kujazwa na waandishi wa habari pamoja na wafanyakazi walio kwenye vyombo vya habari.


Kamati iliyopewa jukumu hilo ina wajumbe wafuatao: Tido Mhando (Mwenyekiti), Dkt. Rose Reuben (Makamu Mwenyekiti), Mobhare Matinyi (Katibu), Sebastian Maganga, Richard Mwaikenda, Bakar Machumu, Joyce Mhavile, Kenneth Simbaya na Jacqueline Woiso


Mjumbe wa Kamati, Sebastian Maganga akiongoza kikao cha kukusanya maoni ya kutathmini hali ya uchumi wa vyombo vya habari na waandishi wa habari katika  Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Novemba 9, 2023, hicho. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati, Dkt Rose Reuben
Mhariri wa Habari Mkongwe ambaye ni Mwanachama wa TEF, Jesse Kwayu akitoa maoni yake.
Mwanachama wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Yassin Sadick akitoa maoni.
Mhariri wa habari mkongwe, Joseph Kulangwa akichangia maoni kwenye kiako hicho.
Wajumbe wa Kamati, Maganga na Dkt Rose wakijadiliana jambo wakati wa kikao hicho.
Mwandishi wa habari mwandamizi ambaye pia ni mwanachamaw a Chama Cha Waandishi wa habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Beatrice Moses akitoa maoni yake.Kushoto ni Khadija Kalili Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Blogu Tanzania (TBN).

Sehemu ya wadau wa habari wakiwa kwenye kikao hicho.














 IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana