Featured

    Featured Posts

HIJA YA CHANZO HALISI MOTO, MAHUJAJI WA MATAIFA YA NJE IKIWEMO MAREKANI WAANZA SAFARI KUJA TANZANIA, KURINDIMA DISEMBA 31, 2023, UWANJA WA LAKE TANGANYIKA KIGOMA MWISHO WA RELI

Na Bashir Nkoromo, Tegeta
Zikiwa zimesalia siku zisizozidi saba kufanyika Ibada ya Hija ya CHANZO HALISI, Mahujaji kutoka Mataifa mbalimbali duniani ikiwemo Marekani wameanza safari kutoka katika nchi zao kuja Tanzania kwa ajili ya kufika mkoani Kigoma kushiriki Hija hiyo.

Ibada ya Hija hiyo ambayo kufanywa na Uzao (waumini) wa Kanisa Halisi kila mwaka, mwaka huu itafanyika katika Uwanja wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma 26 Thebeti 1Majira Halisi, sawa na Jumapili, Disemba 31, 2023 kwa Kalenda ya Gregory.

Akizungumza jana katika Ibada iliyofanyika Makao Makuu ya Kanisa Halisi, Tegeta Namanga Jijini Dar es Salaam, Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi Ndani na Nje ya Tanzania BABA HALISI, alisema, Mahujaji kutoka mataifa ya nje walianza safari jana (juzi) kuja Tanzania.

"Sasa tufanye shukurani kusimamisha Hija Moja Halisi maana imeshaanza. Boston (Marekani) wameanza kuja. Jana (juzi), nilitumiwa kuiona tiketi yao, kwa hiyo kwa kuwa mahujaji wameshaanza safari ni kwamba Hija ndiyo imeanza", akasema BABA HALISI na kuongoza shukurani hiyo.

Dawati la Hija la Kanisa Halisi,  limetaja baadhi ya nchi za nje watakakotokea Mahujaji kuwa ni pamoja na Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Msumbiji, Zambia, Malawi na Congo, DRC, na kwamba safari ya Kigoma baadhi wataianzia Makao Makuu ya Kanisa Halisi, na wengine wataenda moja kwa moja.

"Wapo watakaenda Kigoma kwa usafiri wa ndege na mabasi ya kukodi na wengine kwa treni yenye jumla ya mabehewa 12, ambayo itaanzia Dar es Salaam, na itakuwa ikisimama mikoa ya Morogoro, Dodoma na Tabora kubeba Mahujaji wa mikoa iliyopo karibu na mikoa hivyo. Treni itaondoka Dar es Salaam Ijumaa, Thebeti 24 1Majira Halisi (Disemba 29, 2023)", akasema Ofisa katika Ofisi ya Hija.

KWA NINI KUNA HIJA MOJA HALISI?
Katika Ibada hiyo ya jana BABA HALISI alikumbusha kwa nini hasa Hija ya CHANZO HALISI inafanyika Tanzania mkoani Kigoma, tofauti na ilivozoeleka kwamba Hija Mashariki ya Kati.

"Kwa mujibu wa Mithali 8:14-30, ufahamu una kila kitu ambacho kila mmoja anahitaji", akasema BABA hALISI na kufafanua; "Katika majira saba zilizopita, wote tulitegemea ufahamu ulioanzia Mashariki ya Kati ndiyo maana tunasoma katika Matendo. 8:27- habari za Waziri wa fedha wa Kushi wakati ule akiwa anaenda Yerusalemu kuangalia mahali ufahamu uliokuwepo wakati huo, ulipoanzia.

Kanisa Halisi tunategema ufahamu ulioanzia Tanzania kwenda Mataifa mengine yote (Mathayo 21:43). Hii ni baada ya Sauti ya Chanzo Halisi kusikika mara Nne, hapa Tanzania, mwaka 2003, 2015, 2019 na 2020. Maana sauti ndiyo Chanzo cha ufahamu".

KWA NINI KIGOMA
BABA HALISI pia akafafanua kwa nini Hija ni Kigoma, akasema; "Utakuwa unajiuliza, kwa nini hatuendi Mwanza, Arusha, Dodoma, Mtwara, Ruvuma au mikoa mingine tunaenda Kigoma? Ni hivi kule Kigoma Amerika, Australia, Newsland na mataifa ya Afrika watakuja".

"Sauti ya majira ya sita Adamu wa Pili Sauti aliisikia Kigoma mwaka 2003, Sauti ya majira ya saba miaka 1000 aliisikia Kigoma, Majira Saba za Waliotumwa zikawa zimeisha. Sauti Mpya ambayo ilikuja ikiwa zaidi ya Sauti zote zile saba iliyotusha Korongo ilisikika 2019 Kigoma. Hata Sauti ya Moyo iliyokuja kuzima janga la UVIKO 19 ilisikika Kigoma 2020", akaeleza BABA HALISI.

BABA HALISI akasisitiza zaidi kwamba hata kipindi cha mwaka 862 Dk. Livingstone alifika Bagamoyo akasema siyo hapo, akaenda Tabora nako akasema siyo penyewe, ndipo akaenda mpaka Ujiji, kumbe alikuwa anatafuta Sauti, ila ilikuwa siyo majira yake.

"Wamishenari wa Kipentekoste kutoka Sweden, walisafiri hadi eneo la Tazengwa Tabora, wakaanzisha misheni lakini baada ya kuona sipo wakaondoka hadi Kigoma, hapo wakajenga hiyo misheni, nao walikuwa wanatafuta Sauti.

Waarabu wa Karne ya kumi nao walifika Bagamoyo hadi Dar es Salaam hata wakapaita Bandari ya Salama, baadaye wakagundua bandari Salama siyo hapo ni Ujiji, na wao walikuwa wanatafuta Sauti, pia Wajerumani walipojenga Makao Makuu ya Germany East Africa kule Kigoma walikuwa wanatafuta Sauti ila ilikuwa siyo majira yake.

Kwa hiyo, Hija hiyo ni kwa Watu wote, ili mradi wawe na CHANZO HALISI (Muumba) ndani yao, kwa kuwa Kanisa Halisi la Mungu Baba lipo kwa ajili ya wote na mataifa yote bila kubagua dini maana kila Hija hiyo inapofanyika huachilia baraka na utajiri kwa kila mtu".

Hija iliyopita na kuhudhuriwa na maelfu kwa maelfu kutoka mikoa ya Tanzania Bara, Zanzibar na Nchi za Nje, ilifanyika Januari 27, 2023 au 24 Thebeti 1Majira Halisi, kwa kalenda ya Kabla ya Uharibifu inayofuatwa na Kanisa Halisi na kama ilivyokuwa hiyo iliyopia, ya mwaka huu (Kwa kalenda ya Kanisa Halisi) pia itafanyika Uwanja wa Lake Tanganyika, kuanzia saa 8 mchana hadi saa 11 jioni.

Kwa mujibu wa BABA HALISI pamoja na maelfu ya Mahujaji viongozi na watu mbalimbali walioalikwa wakiwemo wa dini mbalimbali na wasiokuwa wafuasi wa Kanisa Halisi watakuwepo wakati Ibada ya Hija hiyo itakapokuwa inasimamishwa rasmi.

Msafu (Kiongozi) Mkuu wa Kanisa Halisi la Mungu Baba BABA HALISI akieleza kuhusu Hija ya CHANZO HALISI Kigoma, katika Ibada iliyofanyika jana, Jumapili Disemba 24, 2023, Makao Makuu ya Kanisa hilo, Tegeta Namanga Jijini Dar es Salaam.

Tafadhali msikilize Baba Halisi akieleza kwa nini kuna Hija Halisi halafu utazame picha za Ibada ya jana👇

 

PICHA MOTOMOTO ZA IBADA YA JANA👇

Mwimbaji wa nyimbo wa kumbo za kumuinua CHANZO HALISI, akiongoza kuimba kumkaribisha BABA HALISI kupanda utajirishoni kuongoza kuongoza Ibada, Makao Makuu ya Kanisa Halisi Tegeta Namanga jijini Dar es Salaam, jana.
Wapiga vinanda wakikoleza wimbo huo wakiwa katika fulana zao zenye ujumbe 'Bila Chanzo Halisi hutoboi".
BABA HALISI akipiga makofi kufurahia wimbo huo baada ya kupanda utajirishoni.  Kushoto ni Mama Halisi.BABA HALISI akiucheza wimbo huo, huku mbele yake 'Mtekeleza Sauti' kutoka Star tv naye 'akijimaliza' kucheza pia wimbo huo.
'Mkekeleza Sauti' kutoka Star tv ambaye alikuwa akiongoza Matangazo Mubashara ya Ibada hiyo, akimkaribisha BABA HALISI kuanza kuongoza Ibada.
BABA HALISI akianza kuongoza Ibada hiyo kwa kuinua Shukurani kwa CHANZO HALISI kuibariki Ibada hiyo na watu wote.
Mama Halisi, Mnara Mmoja Halisi na Udhihirisho Halisi wakipokea Shukurani iliyokuwa ikiachiliwa na BABA HALISI.
Moja Halisi na Kanisa wake (mke wake) waipokea Shukurani hiyo. Kulia ni Mama Halisi.
Baadhi ya Uzao na Watekeleza Sauti wakipokea Skhukurani hiyo.
BABA HALISI akifanya shukurani kugeuza Maji kuwa Damu Safi Nyeupe ya CHANZO HALISI ili ndiyo isimamie Ibada hiyo.
Moja Halisi na Kanisa wake wakipoea shukurani hiyo. Nyuma yake ni Faida Halisi.
BABA HALISI akinywa maji yakiwa tayari yamekuwa Damu Safi nyeupe ya CHANZO HALISI baada ya kuyafanyia shukurani. Kushoto ni Mama Halisi na Mnara Mmoja Halisi.
BABA HALISI akinyunyiza Damu safi Nyeupe ya CHANZO HALISI kuzunguka utajirisho, baada ya kunywa.
BABA HALISI akifanya shukurani baada ya kunyunyiza Damu Safi nyeupe utajirishoni kubariki Ibada hiyo.
Somo la leo litahusu Hija Halisi, nitaenda haraka haraka kidogo maana ni ndefu", akasema BABA HALISI.
BABA HALISI akieleza kwa kirefu sababu ya kuwepo Hija ya CHANZO HALISI na kwa nini ifanyie Kigoma, Tanzania
Baadhi ya Watekeleza sauti wakimsikiliza kwa makini BABA HALISI. kushoto ni Fahari Halisi na Kanisa wake.
Baadhi ya Watekeleza Sauti na Uzao kwa jumla wakimsikiliza BABA HALISI.
Moja Halisi akisoma Kitabu kushajihisha aliyokuwa akifundisha BABA HALISI kuhusu Hija Halisi. Kushoto ni Fahari Halisi na Kanisa wake.
Baadhi ya Watekeleza Sauti na Uzao kwa jumla wakimsikiliza BABA HALISI.
Baadhi ya Watekeleza Sauti na Uzao kwa jumla wakimsikiliza BABA HALISI.
BABA HALISI akiendelea kueleza kwa kirefu sababu ya kuwepo Hija ya CHANZO HALISI na kwa nini ifanyie Kigoma, Tanzania
BABA HALISI akieleza faida ya kutumia Damu Safi Nyeupe ya CHANZO HALISI katika kufanya chochote kifanikiwe. Hapo alikuwa akijiandaa kutumia hiyo Damu Safi Nyeupe kusimamisha shukurani juu ya kuanza kwa Hija Halisi kufuatia Mahujaji wa Nchi za Nje kuanza safari kuja Tanzania kushiriki Hija hiyo Kigoma.
"Ukitaka jambo lolote lifanikiwe tumia Damu Safi Nyeupe ya Chanzo Halisi na siyo Damu Nyekundu", akasema BABA HALISI.
BABA HALISI akiendelea kufafanua jambo kuhusu Hija Halisi.
Kisha akaongoza shukurani ya Kusimamisha Hija hiyo.
Baada ya kufanya shukurani BABA HALISI akaenda kutoa matunda akiwafungulia Uzao na wengine wote kufanya hivyo.
Mama Halisi akitoa matunda.
Uzao wakitoa matunda.
"Wewe matunda yako unaweka wapi?" wakiulizana watoto hawa wakati wakitoa matunda.
Mwimbaji akiimba wimbo wa kumpelekea matunda CHANZO HALISI wakati utoaji matunda ukifanyika.
BABA HALISI akiinua shukurani ya kuwabariki wote kushiriki Hija Halisi.
BABA HALISI akiinua shukurani ya kuwabariki wote kushiriki Hija Halisi.
Uzao wakipokea shukurani hiyo.
Uzao kwa pamoja wakipokea shukurani hiyo.
BABA HALISI akiwabariki wote watakaoshiriki Hija Halisi.
Uzao wakipokea shukurani ya Baraka ya kwenda Hija Halisi.
BABA HALISI akinyunyiza Damu Safi Nyeupe ya CHANZO HALISI utajirishoni kubariki kila mmoja aweze kwenda Hija hiyo.
Uzao wakiwa kwenye Ibada hiyo.
BABA HALISI akiendelea kusisitiza umuhimu wa Hija Halisi.
BABA HALISI akianzisha kuimba wimbo kutukuza Hija Halisi. waimbaji wakaendelea kuuimba.
Uelewa wa Sauti akiongoza kuimba wimbo huo wa Hija Halisi Kigoma.
Mwimbaji huyu naye akapokea kuongoza kuimba wimbo huo.
Wakati huohuo Dawati la Hija nao wakiendelea kusajili Mahujaji.
BABA HALISI akiwatakia kila la heri wote waliokuwa kwenye Ibada hiyo na waliokuwa wakifuatilia kupitia Luninga. lakini kabla ya kuondoka akasema; " Kesho (leo) na Keshokutwa (kesho) msiende Beach kugaragara kwenye michanga au kuogelea baharini, njooni nyoote hapa tutakuwa na 'Family Day", nitafundisha namna ya kujenga familia iliyo bora".
Huyu Ndugu akijiandaa kumsindikiza BABA HALISI kurejea Ofisini baada ya Ibada.
BABA HALISI akiondoka utajirishoni baada ya kuhitimisha Ibada hiyo.
Wasaidizi wakifuatia kuondoka utajirishoni.
Mama Halisi na Mnara Mmoja Halisi wakiondoka Utajirishoni.
Udhihirisho Halisi pia akiondoka Utajirishoni.

ENDS

Bashir Nkoromo/CCM Blog 2023

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana