Featured

    Featured Posts

MAKONDA: WATENDAJI TANECO KWELI MNAJIONA MNASTAHILI KUMWAKILISHA RAIS DK. SAMIA?

Officiali CCM Blog, CCM Lumumba.
Kufuatia Watanzania kukumbwa na adha ya kutopata umeme wa uhakika kwa muda mrefu, Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Idara ya Itikadi na Uenezi Paul Makonda amepaza sauti kuwata Watendaji Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kujitafakari kama kweli wanajiona wanastahili kumwakilisha Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Makonda amepaza sauti hiyo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari, katika Ofisi Ndogo ya makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam, akionyesha kuwa kwa sehemu kubwa adha ya kutopatikana umeme wa uhakika inachangiwa na uzembe wa Watendaji wa Tanesco.

"Swali letu kama Chama tunawauliza Watendaji wa Tanesco, kweli mnapokaa mlipo kelele na haya maumivu, na kilio na sauti za Watanzania juu ya umeme ninyi mnajisikia fahari? na kama mnajisikia fahari mnajiona mstahili kweli kumwakilisha Mheshimiwa Dk. Samia? Kwamba, naam wakitazama kwenye utoaji wa hiyo huduma mnafaa au mnasubiri tena avunje bodi atengue, ateue?

Huku siyo kumtendea haki Rais wetu na Mwenyekiti wetu wa Chama. Zipo sababu zinajulikana lakini zipo zipo sababu nyingine za uzembe tu, za uzembe tu. Unapoona mtendaji anatoa maelezo yale, mvua zinazoonyesha mvua zote hazipiti huku, amekaa ofisini.

Toka Ofisini utuonyeshee ukiwa kwenye saiti wananchi aone unachosema ndicho chenyewe? Unapokaa ofisini na kutopa maelezo upo ofisini haupo saiti unatengeneza picha na mtazamo tofauti.

Kwa hiyo, kwa kweli pamoja na jitihada ambazo mwenyekiti wetu anazichukua, pamoja na maelekezo mazito anayofanya na maamuzi magumu ya kuvunja mpaka bodi, Chama kingetaka kuwauliza Tanesco, je mnaona mnafaa kumuwakilisha Dk samia?.

Kama leo hii Watanzania wakipiga kura, sekta yenu kitengo chenu taaasisi yenu ingepata asilimia ngapi za kutuongezea ushindi CCM? Na sasa wamemuahidi Mheshimiwa Rais ya kwamba Januari, kinu cha kwanza kinaanza kufanya kazi, ni matumaini yetu ahadi waliyoitoa kwa Mwenyekiti wetu wa Chama iwe ahadi thabiti. hakuna kulala...", akasema Makonda.

MSIKILIZE MAKONDA HAPA👇

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana