 |
| Toleo la kwanza la Gazeti la Uhuru👆 lilizinduliwa Disemba 9, 1961, tarehe ambayo Tanganyika ilipata Uhuru kutoka kwa Waingereza. Hivyo wakati leo tunaadhimisha miaka 62 ya Uhuru wa Tanganyika tunaadhimisha pia miaka 62 ya umri wa Gazeti la Uhuru ambalo lilianzishwa na Chama kilichokuwa cha kupigania Uhuru cha Tanganyika African National Union (TANU), ambacho kilizaliwa rasmi Julai 7, 1954. Viongozi wa TANU wakiongozwa Baba wa Taifa, Hayati (sasa) Mwalimu Julius Nyerere, walitambua umuhimu wa kuwa na chombo watakachomiliki katika kutangaza sera na malengo ya Chama. Habari kubwa iliyoongoza katika ukurasa wa kwanza katika Toleo la kwanza la Uhuru, ilikuwa na kichwa cha habari; ‘BENDERA IMEPANDA. UTUMWA UMEKWISHA’ . #uhuruonline #UhuruUpdates #ukwelidaima #KAZIIENDELEE |
Author Name
Author Description!
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment