Na Yahya Msangi, Togo
Ukiona unanyanyaswa haswa kwenye ofisi ya umma ujue una sifa ya kunyanyaswa. Kuna kitu unakosea.
Ili usinyanyaswe kwenye ofisi ya umma weka nia kuwa "sitakubali kunyanyaswa kwenye ofisi ya umma". Wataogopa kukunyanyasa.
Kuna imani moja potofu ambayo ukishaiweka kwenye ubongo wako utanyanyasika. Imani hiyo ni hii "kila mtumishi serikalini ni mmbaya hivyo hata ukilalamika hutashughulikiwa". Ushaamini watumishi woote ni wabaya. Inafanana na kuamini "polisi woote wala rushwa". "Mahakimu na majaji woote wala rushwa" au "Wahaya woote wahuni" ama. "Wanaijeria woote matapeli".
Exception ni wachaga. Kweli woote ni wezi (zingatia)😆. Wizi umepungua mikoani kipindi hiki 😀😆.
Siku zote kumbuka katika kundi la waovu wapo watu wema wengi kuliko waovu.
Nikupe kisa changu Cha passport:
Kuna kipindi kupata passport Tanzania ilikuwa mbinde. Na ukifika ofisi zao ungeona rushwa waziwazi.
Nilipoenda kutafuta passport yangu ya kwanza nilikuta hali hii. Ilikuwa miaka 30 iliyopita. Mtumishi mhusika anakuelekeza ukamuone mtu aliye nje akushughulikie! Unaelekezwa uende kwa mtu ambaye si mtumishi. Enzi Ile anakudai 5000/= za "kishika uchumba" ndio akushughulikie. Shughuli yenyewe ni kujaza form ya maombi, kupiga picha na kupata kiapo lakini wanafanya iwe ngumuuuu.
Basi kila anayeelekezwa anapewa kikaratasi chenye namba anaenda kumuona asiye mtumishi.
Ilipofika zamu yangu nikakataa. Nikamwambia "yule si mtumishi wa umma". Baradhuli yule akanitazamaaaa. Akaniambia "pisha wenzako wewe hutaki passport". Nikamwambia "kwenye foleni sitoki bila kulipa form za kuombea passport". Akamuita askari. Akataka askari aniondoe. Mimi nikagoma. Yule askari akanywea. Lakini baada ya kelele kibao. Kelele kubwa zilitoka kwa waliokuwa nyuma yangu kwenye foleni. Eti nawapotezea muda. Ukiwatazama wengi sura za nje!
Ikabidi Supervisor atoke kuulizia kulikoni? Yule mtumishi akadai naleta fujo. Pakatokea mzee mmoja ambaye naye alikerwa akamwambia yule supervisor "huyu kijana hajaleta fujo ila amekataa kwenda kule nje kupata huduma". Supervisor akaniita ofisini kwake. Akanipa form nikaijaza. Akaniambia nikalipie . Enzi ile ilikuwa shs 500. Nikalipia. Nikaunganisha na viapo . Nikampa akanipa risiti na tarehe ya kuja kuchukua passport. Yule supervisor akaniambia "hapa kuna syndicate kubwa. Ila kijana umevuka".
Nikaondoka nikawaacha wale wapumbavu wanaendelea kuliwa.
Hiyo ilikuwa miaka 30 iliyopita.
Kipindi hicho watumishi hasa Immigration Dept walikuwa na kibri cha kutisha. Lakini nilikataa kunyanyaswa.
Iweje wewe leo ukubali?
Always kumbuka: Ndani ya kila taasisi kuna watu wema wengi tu. Ukigangamala watakusaidia. Ila ukishaamini wewe ni wa kunyanyaswa utanyanyasika mpaka ukome.
YAHYA MSANGI.
Post a Comment