Na Bashir Nkoromo, CCM Blog, Morogoro
WAKATI wa mchakato wa maandalizi ya matayarisho ya uwezeshaji mafunzo ya Mtaala ulioboreshwa, wapo wataalam wengi waliofanikisha mchakato huo kufikia matokeo chanya kama inavyoshuhudiwa sasa.
Miongoni mwa jopo katika mchakato wa maandalizi hayo ya matayarisho ya Uwezeshaji mafunzo ni Dk. Khalid Sallah, ambaye bila shaka kutokana na kuwa ari ya kujituma na kulitumiia taifa kwa ufanisi wakati wote aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa jopo hilo la wawezeshaji Kitaifa.
Akizungumza na mwandishi wa Official CCM Blog, mjini Morogoro hivi karibuni, alisema Mtaala huo ulioboreshwa mwaka 2023 ni bora zaidi kwa sababu umeachana na maudhui na mambo yote yaliyopitwa na wakati na badala yake na yaliyomo sasa ni yanayokwendana na wakati yakizingatia mahitaji ya dunia ya sasa katika nyanja zote za kimaisha na uongeza kuwa maudhui yote yaliyokuwa yanajirudia rudia katika masomo yameondolewa.
Dk. Sallah alisema mabalidiko katika elimu ya awali na elimu ya msingi ni miongoni mwa mambo yaliyomo katika mtaala huo mpya, aisema ni mabadiliko ambayo yatawezesha shughuli za ufundishaji na ujifunzaji kuwa na tija na kukidhi mahitaji ya ufundishaji na ujifunzaji.
Aliipongeza sana Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi mahiri wa Rais wa Awamu ya Sita Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwezesha fedha na rasilimali zote muhimu zilizofanikisha shughuli za ukusanyaji maoni, uchambuzi na uandishi wa Mtaala.
Dk. Sallah, aliipongeza pia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia chini ya Prof. Adolf Mkenda, TAMISEMI (PO-RALG) chini ya Mohamed Mchengerwa na TET chini ya Dk. Aneth Komba kwa kuwezesha upatikanaji wa wawezeshaji mahiri kitaifa ambao wameonesha uwezo, ari, utashi, msukumo na umahiri wa kuhakikisha kuwa mafunzo kuhusu Mtaala Mpya/ulioboreshwa yanawafikia walengwa kama yalivyopangwa.
Katika mfululizo wa pongezi Dk. Sallah, alimpongeza sana Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dk. Aneth Komba kwa usimamizi mahiri wa kuhakikisha shughuli zote kuhusu Mtaala Mpya zinakamilika hatua kwa hatua kama zilivyopangwa kwa kushirikiana na wakurugenzi wengine wakiwemo Mkurugenzi wa idara ya mafunzo TET Dk. Fika Mwakabungu, Mkurugenzi ldara ya Ukuzaji na Uendelezaji wa Mitaala Dk. Godson Lema pamoja waratibu na viongozi wengine wa TIE.
Kuhusu elimu yake, Sallah alisema ana Shahada ya Udaktari wa Falsafa ya Uongozi katika Elimu (Ph.D) ya UK, Masters (MA.Ed) ya University of Dar es Salaam na B.A.Ed ya Muslim University Morogoro.
Upande wa siasa, Dk. Sallah alisema ni kada kindakindaki wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amewahi kuwa Mwenyekiti wa tawi la CCM na pia amewahi kuwa Katibu Mwenezi wa tawi akiwa anasoma Chuo Kikuu Shahada ya kwanza na shahada ya pili.
Dk. Sallah, alisema mwaka 2020 Sallah aligombea Ubunge kupitia CCM Jimbo la Singida Kaskazini na wakati wa mchakato wa kura za maoni kura hazikutosha.
Alisema, kwa sas ni Mkufunzi wa Chuo Cha Ualimu Mhonda na anaendelea kuitumikia Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia.
Post a Comment