Featured

    Featured Posts

JUMUIYA KUU YA WABAPTIST TANZANIA YAMPONGEZA RAIS SAMIA


Na Lydia Lugakila,

Mwanza


Jumuiya kuu ya Wabaptist  Tanzania  imemshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuli ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kujenga miundombinu mingi ikiwemo shule za msingi na sekondari na vituo vya Afya katika maeneo mengi hapa nchini.


Pongeza hizo zimetolewa na Mchungaji Barnaba Michael Ngusa ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya kuu ya Wabaptist Tanzania kwa niaba ya Jumuiya hiyo kupitia ibada ya kumsimika Mchungaji Peter Deus Mabawa iliyofanyika Januari 21,2024 katika kabisa la Baptist Nyamanoro Mkoani Mwanza.


Mchungaji Barnaba alisema Rais Samia amewapambania Watanzania na kuwajali katika sekta mbali mbali ikiwa ni pamoja na kujenga na kuboresha miundombinu mingi akiwa halali kwa ajili ya Nchi yake ambapo aliwaomba Watanzania na waumini wa madhehebu mbali mbali hapa Nchini kuzidi kumuombea kiongozi huyo.


Aidha katika hatua nyingine mchungaji Michael alimpongeza Rais Samia,Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa kwa jitahada zao za  kuwarejeshea ardhi Wananchi waliodhurumiwa huku pia akimpongeza  Waziri wa Ardhi Jery Silaa kwa kusimamia vizuri zoezi wa urejeshwaji wa ardhi katika mikoa mbalimbali ikiwemo  Mwanza katika wilaya ya Ilemela ambapo tayari Wananchi wamerejeshewa ardhi zao. 


"Tunamshukuru Mungu na Viongozi wetu imeundwa kamati inayoshughulikia urejeshwaji wa ardhi kwa Wananchi ambapo Pia nako Mkoani Dodoma Wananchi wengi wamerejeshewa ardhi na kupewa hati za umiliki wa Ardhi katika kanisa la Moravian" alisema mchungaji huyo.


Aidha kupitia ibada hiyo  mtumishi huyo wa Mungu aliiomba Serikali kuboreshe baadhi ya miundombinu inayoonekana kusua sua katika baadhi ya maeneo ikiwemo umeme na maji huku akiomba pia zoezi la kurejesha na kutoa hati za umiliki wa ardhi liendelee Nchi nzima ili Wananchi waweze kupata mahali pa kujenga nyumba zao, kupata chakula kutokana na mashamba yao.


Mchungaji Michael alitumia nafasi hiyo kuwaasa waumini wa kanisa hilo kuishi kwa misingi na miongozo ya neno la Mungu na kuachana na mienendo isiyofaa katika kazi ya Mungu.


Alisema kuwa Kanisa hilo litawashughulikia baadhi ya  watu walio nje ya kanisa wenye nia ya kuvuruga kanisa pia kuchonganisha Kanisa hilo na Serikali na jamii na kuleta migogoro katika kazi ya Mungu.


Akiwaongoza waumini hao kupitia neno la Mungu alisema kuwai Viongozi wa kanisa hilo wanapaswa kuwaongoza waumini kwa kutumia neno la Mungu, na kuwa ni vyema waumini waishi kulingana na mafundisho ya kweli ya neno la Mungu na si kuenenda kinyume na matakwa ya Mwenyezi Mungu.

 

"Wakristo ni barua ya Kristo yenya sifa njema iliyotumwa ulimwenguni, ili ulimwengu uisome hivyo watu waache matendo maovu watende mema alisema" mchungaji Barnaba.


Mtumishi huyo aliongeza kuwa Kanisa linatakiwa liwasaidie baadhi ya watu walioingia Kanisani na kutengeneza migogoro na kuwachonganisha viongozi wa Kanisa na waumini ili waichukie serikali inayoongozwa na Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan huku akiiomba Serikali kuwashughulikia baadhi ya waumini au watu wanaoleta migogoro na migongano ikiwemo ya kimaslahi na kimadaraka katika nyumba za ibada.


Ikumbukwe kuwa Ibada ya kumsimika Mchungaji Deus Peter Mabawa ilifanyika ikiwa ni kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na  Mchungaji Isaac Madeleke aliyefariki miaka miwili iliyopita.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana