Featured

    Featured Posts

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MABALOZI WATATU WAPYA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

Ikulu, Dar es Sallaam
Makamu wa Rais  Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na mabalozi watatu wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Wa kwanza alikuwa Balozi mpya wa Misri hapa nchini Gaber Mohamed Abulwafa Balozi mpya wa Misri ambaye alifika kwa lengo la kujitambulisha na pia kuzungumzia mambo mbali mbali ya kuimarisha uhusiano baina ya nchini  mbili ambao ulianzishwa na waliokuwa marais wa nchi hizi, Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais Gamal Abdel Nasser Hussein wa Misri.
“Misri itaendelea kutoa ushirikiano katika masuala ya Elimu, Afya na masuala ya teknolojia ya ujenzi wa miundombinu yenye tija kwa mataifa haya mawili” alisema Balozi huyo.
Balozi huyo mpya wa Misri aliahidi kusimamia miradi yote ambayo ipo kwenye makubaliano baina ya Serikali hizi.
Makamu wa Rais alimpongeza na kumkaribisha Tanzania pamoja na kumhakikishia ushirikiano mzuri katika kazi zake akiwa hapa nchini na kumueleza kuwa kwa miaka mingi uhusiano kati ya Misri na Tanzania umezidi kuimarika.
Balozi wa Pili kukutana na kuzungumza na Makamu wa Rais alikuwa ni Francisca Pedros, Balozi mpya wa Hispania hapa nchini ambaye Makamu wa Rais alimpongeza kwa kuwa Balozi wa kwanza mwanamke kuteuliwa kuja kuitumikia nchi yake hapa nchini.
Mwingine ni Balozi wa Ethiopia nchini Yonas Yosef Sanbe ambaye alimueleza Makamu wa Rais furaha yake ya kuwa hapa na kuona namna mahusiano ya nchi hizi mbili yameboreka ambapo alisema kuwa
“Nafarijika kuona namna ambavyo wanawake wanapewa nafasi za juu katika uongozi katika nchi hizi mbili”
Makamu wa Rais pamoja na mambo mengine alimpongeza Balozi huyo wa Ethiopia kwa kuwa Balozi wa kwanza mwenye makazi yake hapa Tanzania.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana