Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo Mhandisi Sylvester Simfukwe (wa pili kushoto) akimpa maelezo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle (wa tatu kushoto) wakati alipotembelea karakana ya Mt. Depot kukagua mashine ya kisasa ya kukagulia magari iliyofungwa katika karakana hiyo. Kushoto ni Meneja wa karakana hiyo Mhandisi Alex William.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle (wa tatu kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo Mhandisi Sylvester Simfukwe (wa pili kushoto) wakati alipotembelea karakana ya Mt. Depot kukagua mashine ya kisasa ya kukagulia magari iliyofungwa katika karakana hiyo ili kurahisisha utendaji kazi. Kushoto ni Meneja wa karakana hiyo Mhandisi Alex William
Gari linaonekana likiwa limenyanyuliwa juu na mashine ya kisasa (3D Wheel Allignment) tayari kwa kuanza kukaguliwa, mashine hiyo ya kisasa imefungwa katika karakana ya TEMESA Mt. Depot Keko Jijini Dar es Salaam. Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA una mpango wa kufunga mashine nyingine kama hizo katika karakana za mkoa wa Mwanza na Dodoma.(PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO - TEMESA)
Post a Comment