Featured

    Featured Posts

SERIKALI YAWATOA HOFU WAKULIMA WA ZAO LA PAMBA NCHINI

NA SALVATORY NTANDU
Serikali imewahakikishia soko wakulima wa pamba katika mikoa yote inayolima zao hilo kwa kufungua masoko katika maeneo yao ili waweze kuuza kwa bei elekezi ya shilingi elfu mmoja na mia mbili.

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Kassim Majaliwa baada ya kutembelea kiwanda cha Kuchambua pamba cha Fresho mkoani Shinyanga na kujionea hali halisi ya ununuzi wa pamba kutoka kwa wakulima unaofanywa na Kampuni ya Fresho Investment Company Limited.

Amesema pamba yote iliyozalishwa na wakulima wa katika msimu huu wa kilimo  itanunuliwa kwa bei elekezi ya shilingi elfu 1,200   hivyo wakulima wasiwe na hofu makampuni mbalimbali nchini yanaendelea na ununuzi wa zao hilo.


Amefafanua kuwa anaendelea ziara kwenye mikoa inayolima pamba lengo la kufuatilia mwenendo wa masoko ya pamba na katika mkoa wa  Shinyanga ameshuhudia namna zoezi la ununuzi linavyoendelea unaofanywa na kampuni ya fresho.

Katika hatua nyingine Waziri Majaliwa amempongeza  Mkurugenzi Kampuni ya Fresho Fredy Shoo kwa  kununua pamba kama serikali tunakushukuru  na tutakulinda,hatutakuangusha. Hapa kuna mkuu wa mkoa,ukipata tatizo usisite kumuona.

Mbali na hilo  Majaliwa amewapongeza wakulima kwa kuzingatia usafi kwenye pamba kwa kuachana na tabia ya kuweka maji,mchanga,mafuta na takataka mbalimbali zinazosababisha pamba ichafuke na kuchangia sasa pamba ya Tanzania inapendwa duniani kote.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana