BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni limemchagua Mhe.George Manyama kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Naibu Meya wa Halmashauri hiyo kwa awamu ya nne tangu mwaka 2016. Uchaguzi huo umefanyika leo (jana) katika baraza maalumu la madiwani la robo ya mwaka ambapo jumla ya wajumbe 21 ambao ni madiwani walishiriki uchaguzi huo.
Akitangaza matokeo hayo, Katibu tawala wa Halmashauri hiyo Bi Stella Msofe amesema kuwa idadi ya kura zilizopigwa ni 21 kulingana na wajumbe wa baraza hilo kutoka vyama vyote vyenye madiwani katika baraza hilo. Msofe amemtangaza Mhe. Manyama kutoka CCM kuwa mshindi wa nafasi hiyo ya Naibu Meya kwa kupata kura 13, huku mpinzani wake Mhe. Phares Lupomo kutoka chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema akipata kura nane.
Awali wagombea hao wawili walipata nafasi ya kunadi sera zao kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo ikiwa ni Toggle screen reader support.
Post a Comment