Endapo hatua zisipochukuliwa za saratani ya matiti inaweza kushika namba moja kwa kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa nchini.
Hayo yanesemwa na Mkurugenzi wa huduma za Kinga ya Saratani katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) Dkt. Crispian Kahesa alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mwezi wa uhamasishaji , uelimishaji na uchunguzi wa saratani ambao huadhimishwa kila mwezi oktoba kila mwaka.
“Idadi ya saratani ya matiti inaonekana kuongezeka nchini ambapo hivi sasa wanawake wenye umri kuanzia miaka 20 na kuendelea nao wanagundulika kuugua ugonjwa huu”. Alisema Dkt. Kahesa.
Alisema kuwa endapo hatua zisipochukuliwa saratani hiyo itazidi kuwa tishio zaidi na kwamba idadi kubwa ya wagonjwa wanaofika hospitalini hapo wanatoka katika maeneo ya mjini ambapo mkoa wa Dar es salaam unaonekana kuongoza.
“Tathimini ya miaka 10 iliyopita saratani hii ilikua inashika nafasi ya tano ,hivi sasa ni ya pili kwa kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa,zamani tulikua tunawaona wagonjwa kuanzia miaka 55 ukashuka hadi miaka 50 na sasa tunaona hadi wenye umri wa miaka 20”.
Dkt. Kahesa alisema kuwa kwa mwaka huu pekee wameweza kuona wanawake 1443 ambapo kati ya 342 wamekutwa na uvimbe 170 walikuwa na dalili za awali za saratani.
Kwa upande wa saratani kwa wanaume Dkt. Kahesa alisema kuwa saratani hiyo huathiri asilimia moja kwa wanaume hata hivyo kwa upande wao ni hatari zaidi na endapo isipogundulika huweza kuathiri mapafu yao kwa haraka.
“Saratani hii huathiri wanawake zaidi kuliko wanaume kwa asilimia 99 na wanaume ni asilimia 1 tu,ambapo dalili kwa wanaume ni tofauti kidogo na wanawake,hivyo kwa mwanaume ni rahisi kugundua kuliko mwanamke kwa kuwa kifua chake kina mafuta mengi.
Aliongeza kuwa kati ya wanawake 170 waliofanyiwa vipimo zaidi ya 68 waligundulika na vivimbe ambavyo ni ugonjwa wa saratani.
Hapa nchini saratani ya shingo ya kizazi inaongoza ikifuatiwa na saratani ya matiti,saratani ya njia ya chakula,saratani ya tezi dume na saratani nyingine ni zile zinazoathiri mfumo wa kinga.
Post a Comment