Ndege za kivita zenye mfungamano na kundi kwa jina la jeshi la kitaifa la Libya linaloongozwa na Kamanda Khalifa Haftar jana Jumatano ziliushambulia mji wa Misrata kaskazini mwa nchi hiyo.
Ndege hizo zimekilenga pia chuo cha mafunzo ya anga katika mji huo. Hadi sasa kuna taraifa iliyotolewa kuhusu hasara na maafa yaliyosababishwa na mashambulio hayo huko Misrata. Kundi kwa jina la jeshi la kitaifa la Libya linaloongozwa na Khalifa Haftar ambalo kwa miaka kadhaa sasa limekuwa likiyashikilia maeneo ya mashariki mwa Libya kwa uungaji mkono wa Saudi Arabia, Misri, Imarati na baadhi ya nchi nyingine za Magharibi; miezi kadhaa ya karibuni lilisonga mbele upande wa kaskazini mwa Libya. Haftar tarehe nne Aprili mwaka huu aliwaamuru wanamgambo wake waushambulie mji mkuu Tripoli; hujuma iliyokosolewa na na kulaani na jamii ya kimataifa.
Watu zaidi ya 1090 wameuawa na wengine wasiopungua 5700 kujeruhiwa katika mji mkuu wa Libya Tripoli tangu kuanza mashambulizi hayo tajwa ya wanamgambo wanaoongozwa na Khalifa Haftar dhidi ya mji mkuu huo hadi hivi sasa.
Post a Comment