Vyama vya siasa nchini Uingereza hii leo vimezindua kampeni za uchaguzi wa tatu katika kipindi cha chini ya miaka mitano.
Kampeni hizo zinatarajiwa kugubikwa na suala la Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya ama Brexit. Waziri mkuu Boris Johnson amenukuliwa kwenye ukurasa wa Twitter akisema "tulipeleke taifa letu mbele na kufanikisha vipaumbele vya raia." Johnson wa chama cha Conservative ameandika hayo baada ya bunge kuridhia mwito wake wa uchaguzi Desemba 12 katika kura ya jana usiku.
Johnson anaamini kushinda wingi wa kura utakaomuwezesha kuondoa kizingiti cha bunge katika mchakato wa kupitisha makubaliano ya Brexit aliyofikia na Umoja wa Ulaya bila ya kutegemea kura za upinzani.
Post a Comment