Featured

    Featured Posts

ETHIOPIA YAPINGA UPANISHI WA MAREKANI KATIKA MAZUNGUMZO YA BWAWA LA EL NAHDHA

Kuhusiana na suala hilo, wawakilishi wa nchi tatu za Kiafrika yaani Misri, Ethiopia na Sudan wamekutana kwa lengo la kuchunguza mpango huo uliozusha mjadala mkubwa kuhusiana na ujenzi wa bwawa la El Nahdha huko Ethiopia katika maji ya mto Nile. Washington ndiyo iliyokuwa mwenyeji wa kikao hicho kilichosimamiwa moja kwa moja na Rais Donald Trump wa Marekani. Kinyume na madai yaliyotolewa na Marekani, Ethiopia na Sudan zilishiriki katika kikao hicho kwa ajili ya mashauriano na si kikao cha usuluhishi wa Washington.  
Nebiat Getachew msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya thiopia amesisitiza kuwa kikao hicho hakikuwa cha mazungumzo na madai ya Marekani  kwamba ilikuwa mpatanishi katika kikao hicho si sahihi. Getachew amesema nchi yake ilishiriki kikao hicho ili tu kuweka wazi msimao wake; na haiyatambui mazungumzo hayo kama fursa kwa ajili ya kuanza mazungumzo ya kiufundi juu ya mgogoro wa maji ya Mto Nile. 
Nebiat Getachew. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia
 
Ujenzi wa bwawa la El Nahdha huko Ethiopia ambao ulianza mwaka 2011 katika eneo la kilomita 40 kutoka mpaka wa Sudan hivi sasa umeibua hitilafu kati ya Addis Ababa, Cairo na Khartoum. Misri kwa upande wake inaamini kuwa ujenzi wa bwawa hilo ni hatari kwa usalama wake wa maji na inahitilafiana Addis Ababa kuhusu kiwango cha maji yanayoingia Misri kila mwaka kupitia nchi hiyo na namna ya kuyadhibiti katika vipindi vya ukame. Kuhusiana na suala hilo katika miaka ya karibuni vikao vingi vimefanyika kati ya nchi hizo tatu na kutolewa mapendekezo mbalimbali ya kuzipatia ufumbuzi hitilafu zilizopo. Hata hivyo pande husika kwenye mazungumzo zimeshindwa kupata njia ya pamoja ya utatuzi na mwezi uliopita nchi hizo tatu zilifikia hatua ya kutoleana vitisho vya kutumia nguvu za kijeshi baada ya kupamba hitilafu kati yazo.  
Abiy Ahmed Waziri Mkuu wa Ethiopia ameashiria namna nchi yake ilivyodhamiria kukamilisha mradi wa bwawa la El Nahdha na kusema kwamba hakuna nchi yoyote inayoweza kukwamisha ujenzi wa bwawa hilo. Abiy Ahmed amesema: Tunaweza kukusanya mamilioni ya wapiganaji iwapo kutakuwapo na haja ya kupigana vita.  
Abiy Ahmed Waziri Mkuu wa Ethiopia
Wakati huo huo Misri imewasilisha ombi la usuluhishi kutoka nje kufuatia kupamba moto hitilafu kati ya nchi hizo. Pande husika kwenye mazungumzo hayo haziungi mkono pendekezop hilo la Cairo. Hata hivyo Marekani kiwa nchi muitifaki wa Misri na Ethiopia imesisitiza kuwa inaunga mkono mazungumzo hayo kuhusu ujenzi wa bwawa la El Nahdha ili kufikia mapatano  yatakayopelekea kulindwa haki za pande zote na kupatikana ustawi endelevu wa kiuchumi.
Mazungumzo yanaendelea kufanyika huku Sudan na Ethiopia zikiyataja mazungumo hayo kuwa ni kikao tu cha kubainisha maoni yao na zimepinga Marekani kuwa msuluhishi katika mgogoro huo.
Inaonekana kuwa kama Misri, Ethiopia na Sudan zitashindwa kufikia natija ya kuridhisha kuhusu ujenzi wa bwawa wa El Nahdha, kujiingiza baadhi ya nchi ajinabi ikiwemo Marekani kama kadhia hiyo si tu hakutatui mgogoro uliopo bali kutachochea nchi moja dhidi ya  nyingine na kuandaa mazingira ya kutokea vita vya muda mrefu katika eneo hilokwa maslahi ya nchi ajinabi ukiwemo utawala wa Kizayuni wa Israel. 
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana