Na Lydia Lugakila;- Kagera
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Generali Marco Elisha Gaguti amewataka watumishi na taasisi zilizokopa fedha katika Benki ya wakulima ambayo
ilifungwa kuhakikisha wanarejesha fedha hizo ndani ya siku 4.
Akizungumza na viongozi wa chama kikuu cha ushirika mkoa wa Kagera KCU, Chama kikuu cha ushirika wilaya ya Karagwe na kyerwa KDCU amesema amefuatilia na kukuta zaidi ya shilingi bilioni 2 hazijarejeshwa bado zimo mikononi mwa watumishi na taasisi hizo.
Brigedia Gaguti amesema kukopeshwa kwa fedha hizo
bila kufuata utaratibu ndo kulisababisha benki hiyo kufungwa na hivyo kuwataka watumishi hao kutambua kuwa fedha hizo ni za wakulima.
Amesema kuwa atakayeshindwa kurejesha fedha hizo ndani ya siku 4 anatakiwa kujisalimisha kwenye kamati ya ulinzi na usamalama ya mkoa vinginevyo hatua kali za kisheria zitaanza kuchukuliwa dhidi yao.‘’Wapo walioikopa na kusababisha benki hiyo ikafilisiwa hadi ikafungwa fedha hizo lazima zirudi nimefatilia nimeona wako
watendaji wanaendelea na maisha kama kawaida zimo taasisi zinaedelea na maisha kama kawaida huku fedha zilizokuwa za wakulima hazieleweki zilipo’’alisema Brigedia Gaguti.
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa amewataka viongozi wa vyama hiyo kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja wanapata taarifa kuhusu namna ya rasilimali za vyama hivyo zinavyotumika na
namna zinavyowanufaisha wakulima
Post a Comment