Featured

    Featured Posts

CCM YATOA TATHIMINI YA AWALI KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza tathmini yake ya awali kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa uliopangwa kufanyika tarehe 24 mwezi huu, 2019.

Zifuatazo ni ndondoo za tathmini hiyo kulingana na maelezo yaliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole, wakati akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

1. Jumla ya wanachama 930,717 wa CCM  waliomba  kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kupitia CCM kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

2. Wagombea wa CCM wamepita kwenye uteuzi kwa asilimia 99.9

3. CCM ina jumla ya mashina 232,000 nchi nzima na kila shina lina wanachama  takribani 100

4. Wana CCM Milion 15 wamejiandikisha katika daftari la kupiga kura.

5. CCM  iliandaa Wanasheria/ Mawakili 1,250  na kuwasambaza nchi nzima.

6. Kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa zilitolewa miezi 7 iliyopita na kila chama cha Siasa kilipewa.

7. Vyama vya upinzani havikuwekeza kwenye elimu kama Ilivyofanya CCM.

8. CCM imefanya maandalizi ya kutosha kwenye uchaguzi huu.

9. Wagombea wa upinzani wameenguliwa kwa sababu ya ujinga wa wenyewe.

10. TAKUKURU Imfuatilie Mbunge mmoja kutoka Kilimanjaro kwa tuhuma za jinai. Mbunge huyo akaunti yake ilikutwa na sh. Bilioni 1 na zilikuwa mahsusi kuhonga wagombea wa CCM.

11. Polisi ni walinzi wa amani na usalama hivyo hakuna haja ya kujenga dhana ya hofu dhidi yao. Hata mikutano ya CCM huwa Wanaokuwepo.

12. CCM kisheria inayo haki kufuatilia utekelezaji wa ahadi zake ilizotoa wakati wa uchaguzi.

13. Wagombea wote walijaza fomu fupitia mawakili walioajiriwa na CCM. Hakuna mgombea aliyejazia fomu nyumbani kwake akiwa na mkewe.

14. Vyama vya upinzani vina Kazi Moja tu kuichafua nchi yetu.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana