Uzinduzi wa Kitabu na Filamu kuhusu historia ya Reli ya TAZARA umefanyika leo Beijing.
Hafla hiyo ni sehemu ya matukio yanayoendelea ya Kumbukizi ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere yanayofanywa na Chuo Kikuu cha Zhejiang Normal University.
Ujenzi wa Reli ya TAZARA ni moja ya ‘legacy’ ya Baba wa Taifa inayoenziwa nchini China ikiwa ni alama ya urafiki kati ya China na Bara la Afrika.
Katika hafla hiyo Chuo Kikuu cha Zhejiang Normal University kimetangaza dhamira yake kuanzisha kozi ya lugha ya Kiswahili. Vilevile, wameeleza mpango wa kuanzia kituo cha mafunzo ya uongozi kitakachojulikana kama Julius Nyerere Study Centre.
Kituo hicho kitashughulika na tafiti mbalimbali juu ya falsafa za Uongozi Barani Afrika. Rais wa Zhejiang Normal University na Balozi wa Zambia Mhe Winnie Chibesakunda, Mabalozi na Wanazuoni pia wameshiriki hafla hii. Habari/Picha kwa hisani ya Phelista Wegessa
Balozi wa Tanzania nchini China,Mhe.Mbelwa Kairuki akizungumza kwenye hafla ya Uzinduzi wa Kitabu na Filamu kuhusu historia ya Reli ya TAZARA uliofanyika jijini Beijing. Hafla hiyo ni sehemu ya matukio yanayoendelea ya Kumbukizi ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere yanayofanywa na Chuo Kikuu cha Zhejiang Normal University.
Picha ya pamoja wakati wa uzinduzi
Wadau mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye uzinduzi huo
Post a Comment