Featured

    Featured Posts

WAFUASI WA SHEIKH ZAKZAKY WAANDAMANA MJINI ABUJA WAKITAKA KUACHIWA HURU KIONGOZI HUYO

Ofisi ya Sheikh Zakzaky imeandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter ikiambatanisha na picha za waandamanaji kwamba: Maandamano ya wananchi yamekuwa yakifanyika kila siku katika eneo la Garki mjini Abuja yakitaka kuachiliwa huru bila masharti, Sheikh Ibrahim Zakzaky.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, waandamanaji hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu walisikika wakipiga nara za kutaka kuachiliwa huru Sheikh Ibrahim Zakzaky na kuikosoa vikali hatua ya vyombo vya usalama vya Nigeria ya kuendelea kumshikilia kizuizini mwanazuoni huyo.
Sheikh Ibrahim Zakzaky, Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria 
Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe walitiwa nguvuni tarehe 13 Desemba 2015 wakati askari wa jeshi la Nigeria walipovamia na kushambulia Hussainiyah iliyoko katika mji wa Zaria. Katika shambulio hilo, mamia ya Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Nigeria, wakiwemo watoto watatu wa kiume wa Sheikh Zakzaky, waliuawa shahidi.
Baada ya jitihada kubwa, maandamano ya kila pembe na mashinikizo mengi ya ndani na kimataifa, mnamo mwezi Agosti mwaka huu, mahakama ya Nigeria iliruhusu Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe wapelekwe India kutibiwa, lakini kutokana na matatizo na vizuizi vilivyowekwa na maafisa wa usalama walioandamana naye, kiongozi huyo wa kidini pamoja na mkewe waliamua kurudi Nigeria baada ya kukaa India kwa muda wa siku mbili tu pasi na kupatiwa matibabu.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana