Baada ya kuanza mgogoro wa Syria hapo mwaka 2011 na vita vilivyosababishwa na mgogoro huo, Marekani ilikuwa na nafasi muhimu na kuu katika kuundwa na kujitokeza makundi ya kigaidi nchini humo hususan kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh; suala ambalo Washington imefanya jitihada kubwa za klificha kwa kuanzisha kile ilichodai ni muungano wa kupambana na Daesh.
Hata hivyo, Russia kama mpinzani wa kimataifa wa Marekani, imekuwa ikiweka wazi na kufichua uhakika huo. Katika mkondo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema: Aliyekuwa kiongozi wa kundi la kigaidi la Daesh Abu Bakr al Baghdadi alitengenezwa na Wamarekani. Lavrov amesema kuwa, kama habari ya kuuawa Abu Bakr al Baghdadi itakuwa ya kweli basi Marekani itakuwa imemuangamiza mtu iliyemtengeneza yenyewe.
Jumapili iliyopita Rais Donald Trump wa Marekani alitangaza kwamba kinara huyo wa Daesh ameuawa katika operesheni maalumu iliyofanywa na askari wa nchi hiyo katika mkoa wa Idlib, nchini Syria.
Mwaka 2009 Washington ilimwachia huru Abu Bakr al Baghdadi aliyekuwa akishikiliwa katika jela na Abu Ghuraib nchini Iraq na hivyo kumtayarishia mazingira ya kuanza harakati zake. Al Baghdadi alishika hatamu za uongozi wa kundi la kigaidi la Daesh na kufanya mauaji na jinai zisizo na mfano katika nchi kama Iraq na Syria. Sasa na baada ya kumalizika muda wa matumizi ya kikaragosi hicho, jeshi la Marekani limejitokeza mbele na kumuangamiza ili kumzika kaburini kabla yakufichua siri na mahusiano yake na mabwana zake. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran anasema: "Abu Bakr al Baghdadi na vinara wengine wa makundi ya kigaidi katika kanda ya Mashariki ya Kati walitengenezwa na Marekani, kama wanavyokiri Wamarekani wenyewe. Sayyid Abbas Mousavi anasema vikaragosi hao wa Marekakni wana muda maalumu wa matumizi na pale unapomalizika huuawa na kuangamizwa na mabwana zao wenyewe."
Katika mikakati yake ya kutimiza malengo yake kwenye eneo la Asia magharibi, Marekani imekuwa na nafasi muhimu sana katika kuundwa na kuimarika kundi la kigaidi la Daesh. Baada ya kuanza mgogoro wa Syria Marekani ikiwa kinara wa nchi za Magharibi pamoja na washirika wake waliyagama makundi ya kigaidi baina ya magaidi wazuri na magaidi wabaya na hivyo kuhalalisha nafasi yake ya kuyaunga mkono na kuyafadhili makundi "mazuri" ya kigaidi kama Daesh.
Rais Donald Trump amekuwa akidai kuwa Marekani inafanya mikakati ya kuliangamzia kundi la Daesh lakini madai hayo yalikuwa kinyume na ukweli wa mambo. Inaonekana kuwa, Trump amesahau au amejisahaulisha kwamba, katika kampeni za uchaguzi wa rais mwaka 2016 aliitaja serikali ya Barack Obama kuwa ndiyo iliyoanzisha kundi la kigaidi la Daesh. Katika hotuba yake ya Januari 2016, Donald Trump alisema: "Obama na Hillary Clinton sio wakweli na wao ndio waliounda kundi la Daesh. Hillary Clinton na Obama walianzisha kundi la Daesh."
Ukweli ni kwamba, Marekani inanayatumia makundi ya kigaidi likiwemo la Daesh kama wenzo wa kutimizia malengo na maslahi yake. Kwa maneno mengine ni kuwa, japokuwa Marekani inadai kuwa inapambana na Daesh lakini daima mapambano hayo yanafanyika kwa mipaka makhsusi na si kwa ajili ya kuliangamzia kabisa kundi hilo. Kwa sababu hiyo mwezi Februari mwaka 2015 Rais Vladmir Putin wa Russia alisema kuwa: Hatua za kijeshi za Marekani katika eneo al Asia magharibi zimetayariaah mazingira na uwanja wa kushamiri harakati za kundi la kigaidi la Daeh katika nchi za Iraq na Syria.
Kuanzia mwaka 2011 hadi 2014 Marekani ilikuwa ikilihudumia kundi la Daesh na kulifadhili kwa silaha na fedha. Baada ya kundi hilo kuvamia sehemu ya ardhi ya Iraq na kutwaa eneo kubwa la ardhi ya nchi hiyo, Washington na katika kipindi cha utawala wa Obama iliamua kudhibiti harakati za kundi hilo kibaraka na kwa msingi huo mwaka 2014 iliunda muungano wa kimataifa eti wa kupambana na Daesh. Lengo kuu la Marekani kipindi hicho lilikuwa kulilinda kundi hilo kwa ajili ya kutumia wapiganaji wake dhidi ya jeshi na serikali ya Syria na waitifaki wake.
Kwa utaratibu huo Washington inatarajia kwamba, itatumia mabaki ya Daesh ambao inakadiria kuwa wanafikia maelfu kadhaa ya wapiganaji, dhidi ya serikali ya Syria na waitifaki wake au kuwatumia katika operesheni za kigaidi dhidi ya wapinzani wa Washington katika nchi za Syria na Iraq.
Post a Comment