Spika wa Bunge la Wawakilishi la Marekani amesisitiza kufuatiliwa mchakato wa kumsaili Trump na kuwasilisha mpango huo kwa Seneti na kueleza kuwa Trump mwaka ujao wa 2021 hatokuwa rais mpya wa Marekani.
Akizungumza Jumatatu hii na televisheni ya ABC NEWS, Bi Nancy Pelosy ameongeza kuwa, mbali na suala hilo, kuna uwezekano mkubwa wabunge wa chama cha Democrat wakamfukuza White House Trump kupitia kufuatilia mchakato wa kumsaili kabla ya kufanyika uchaguzi wa rais wa mwaka huu na hivyo atakuwa amesailiwa daima.
Spika wa Bunge la Wawakilishi la Marekani amebainisha kuwa wiki hii watatuma mpango wa kumsaili Trump katika Seneti ya nchi hiyo ili kufanyika kikao cha kumhukumu.
Pelosy amesema kuwa kesho Jumanne watakuwa na kikao cha mashauriano katika bunge la wawakilishi na wabunge wenzake wa Democrat kujadili suala hilo. Aidha amesisitiza kuwa kuchelewesha kuwasilisha katika bunge la seneti mpango wa kumsaili Trump kumesaidia kuongeza uelewa wa wapiga kura wa Marekani.
Bunge la Wawakilishi la Marekani tarehe 18 Disemba mwaka jana liliipigia kura ya kihistoria hoja ya kumsaili Donald Trump kwa kutumia tuhuma mbili; mosi ya kutumia vibaya madaraka na pili ya kukwamisha uchunguzi ndani ya Kongresi.
Post a Comment