Featured

    Featured Posts

RAIS MACRON WA UFARANSA ARUSHIANA MANENO MAKALI NA POLISI WA ISRAEL MJINI QUDS

Kwa mujibu taarifa, siku ya Jumatano Rais wa Ufaransa alikuwa anatembelea kanisa la Saint Anne katika mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu na Israel. Kanisa hilo lililojengwa karne kadhaa zilizopita ni milki ya serikali ya Ufaransa na wakati Rais Macron alipofika hapo alirushiana maneneo makali na polisi wa utawala wa Kizayuni wa Israel ambao walikuwa wanataka kuingia katika kanisa hilo kwa nvugu jambo ambalo lilimkasirisha sana Macron ambaye aliwataka watii sheria
Macron alisema lazima polisi hao watii sheria za karne kadhaa za kanisa hilo na huku akionekana kuwa mwenye hasiria aliwahutubu maafisa hao wa Polisi ya Israel kwa kusema: "Sote tunafahamu sheria, sifurahishwi na kitendo chenu mbele yangu. Tokeni nje!
Polisi wa utawala wa Kizayuni wa Israel walikuwa wanataka kuendamana na Macron wakati wa ziara yake ndani ya kanisa hilo la zama za vita vya msalaba.
Macron akiwa amezingirwa na maafisa wa usalama
Macron si kiongozi wa kwanza wa Ufaransa ambaye amekasirishwa na vikosi vya usalama vya utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu suala hilo.
Mwaka 1996 pia, rais wa wakati huo wa Ufaransa Jacques Chirac alikumbana na tatizo sawa na hilo la Macron wakati polisi wa utawala wa Kizayuni wa Israel walipojaribu kumzuia kuwakaribia Wapalestina jambo ambalo lilipelekea atishie kukatiza mara moja safari yake Israel.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana