Azam FC tumepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mke wa Nahodha wetu, Agrey Moris, aliyefariki dunia jana jioni wakati akiwa kwenye harakati za kujifungua.
Tunatoa salamu zetu za pole kwenda kwa familia ya Moris, pamoja na ndugu, jamaa na marafiki na wote walioguswa na msiba huo.
Azam FC tunaungana na familia ya marehemu na tunamuomba Mwenyezi Mungu, awajalie nguvu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.
Bwana ametoa na Bwana Ametwaa, Jina lake lihimidiwe. Amen.
Post a Comment