Vijana wanaoandamana kwa kufanya vurugu nchini Iraq wameshambulia kambi moja ya jeshi la Hizbullah ya Iraq kambi iliopo karibu na uanja wa ndege wa kimataifa wa Najaf na kuchoma moto majengo yaliopo katika kambi hiyo.
Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: wafanya fujo hao wanaopinga serikali ya nchi hiyo walikusanyika katika mji wa Najaf huku wakichoma moto matairi ya gari na kuyasambaza barabarani jambo liliopelekea magari kushindwa kutembea katika barabara hizo.
Miongoni mwa madai yao ni kile kilichotajwa kuwa ni kuto tekelezwa ahadi iliotolewa na serikali yao, ambapo waliamua kufunga ofisi za serikali na kushambulia kambi ya majeshi ya Hizbullah ya Iraq iliopo katika barabara inayokwenda uwanja wa ndege wa kimataifa wa Najaf na kuchoma moto majengo ya kambi hiyo.
Ripoti sahihi zinaonyesha kuwa mji wa Baghdad na miji mingine kadhaa ya Iraq toka mwezi Oktoba mwaka huu ilionekana kufanyika maandamano ya kupinga sistimu ya siasa ya nchi hiyo, kadhalika kudorora kwa huduma za kijamii, ugumu wa kupatikana kwa ajira nchini humo.
Baada ya siku kadhaa ikaonekana katika maandamano hayo ya kisheria kuingia mikono ya maadui wa nchi hiyo ikiwemo mamluki wa ubalozi wa Marekani nchini humo pamoja na vikundi vya kigaidi viliopo nchini humo na kadhalika miengo ambayo yalibadili muonekano wa maandamano hayo ya kisheria na kuwa ya fujo na kuharibu mali za uma, hata kupelekea kufungwa kwa baadhi ya mashule na vyuo vikuu nchini humo.
Post a Comment