Featured

    Featured Posts

KAMATI YA SIASA CCM MKOA WA SHINYANGA YAIPONGEZA SHUWASA KASI YA UJENZI MRADI WA MAJI WA MWAWAZA - NEGEZI

Msimamizi wa Mradi wa Maji wa Mwawaza – Negezi (Mwawaza- Negezi Water Supply Project) Mhandisi Yusuph Katopola (Kulia), akimuonesha Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa hatua iliyofikiwa ujenzi wa tenki la Maji linalojengwa katika kata ya Mwawaza kwa ajili ya mradi wa Maji wa Mwawaza - Negezi. PICHA ZAIDI>BOFYA HAPA

MWANZA, Tanzania
Kamati ya Siasa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Mabala Mlolwa imetembelea Mradi wa Mwawaza - Negezi katika Manispaa ya Shinyanga na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi huo.

Mradi huo wa Maji ya Ziwa Victoria unaosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) kwa kushirikiana na Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) hadi kukamilika kwake unatarajiwa kugharimu jumla ya shilingi Bilioni 2.

Akizungumza leo Februari 11,2020 katika eneo la ujenzi wa Tenki la Maji katika kata ya Mwawaza,Mwenyekiti CCM mkoa wa Shinyanga,Mhe. Mabala Mlolwa ameeleza kufurahishwa na kasi ya ujenzi mradi huo wa maji.

“Niwapongeze SHUWASA kwani naona ujenzi huu wa mradi unaendelea vizuri. Naipongeza serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli kwa kutekeleza kwa vitendo ilani ya uchaguzi ya CCM,kwani wakati wa kampeni za uchaguzi tuliahidi kuwaletea maji safi na salama wananchi”,alisema Mabala.

“Ujenzi wa mradi wa maji kata ya Mwawaza ni sehemu ya ahadi tulizoahidi.Ni matumaini yangu kuwa pindi mradi huu utakapokamilika wananchi wa Mwawaza na vijiji jirani watanufaika na mradi huu wa maji”,alisema Mabala.

Msimamizi wa Mradi wa Maji wa Mwawaza – Negezi, Mhandisi Yusuph Katopola kutoka SHUWASA, alisema SHUWASA inasimamia na kujenga mradi huo wa maji kwa kutumia wataalamu wa ndani “Force account” ambapo Miradi hiyo inahusisha ujenzi wa matenki na mtandao wa maji safi.

Alisema mradi wa maji wa Mwawaza – Negezi (Mwawaza- Negezi Water Supply Project) unatarajiwa kukamilika mwezi Juni mwaka 2020 ukitarajia kunufaisha wananchi wa kijiji cha Mwawaza,Negezi na Bugimbagu na vijiji jirani.

“Mradi huu unahusisha ujenzi wa tenki na mtandao wa maji safi.SHUWASA inaendelea na utekelezaji wa mradi huu ambapo kwa sasa ujenzi wa tenki kwa mradi wa Mwawaza – Negezi umefikia hatua ya ukuta kwa tenki lenye ujazo wa lita 200,000 na hatua ya ufungaji wa nondo za ukuta kwa tenki dogo lenye ujazo wa lita 50,000”,alisema Mhandisi Katopola.

Alisema ujenzi wa matenki unaosimamiwa na SHUWASA kwa kushirikiana na RUWASA unatarajia kugharimu fedha za Kitanzania shilingi Milioni 130 hadi kukamilika kwake.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana