Featured

    Featured Posts

MISRI YATAKA BARA LA AFRIKA LIPEWE HAKI YA KURA YA VETO

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri imesema kuwa, mwakilishi wa nchi hiyo katika Umoja wa Mataifa, Mohamed Idris ametoa ombi hilo sambamba na kuanza kikao cha duru mpya ya mazungumzo ya Baraza la Usalama kuhusu mabadiliko na ustawi ndani ya jumuiya hiyo ya kimataifa.
Taarifa hiyo imesema kuwa, mwakilishi wa Misri katika UN ameashiria makubaliano yaliyofikiwa baina ya viongozi wa nchi za Afrika katika mkutano wa siku chache zilizopita mjini Addis Ababa chini ya uenyekiti wa Misri na kusisitiza kuwa: Cairo inataka bara la la Afrika lipewe viti viwili vya kudumu katika Baraza la Usalama na mamlaka kamili ikiwa ni pamoja na haki ya kura ya turufu. 
Mkutano wa viongozi wa Afrika, Addis Ababa
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lina jumla ya wanachama 15, na wanachama 5 miongoni mwao wana haki ya kutumia kura ya veto.  
Nchi tano zenye haki ya kutumia kura ya turufu ni Marekani, Russia, Ufaransa, Uingereza na China. Nchi hizi hususan Marekani zimekuwa zikitumia vibaya kura hii ya turufu kwa maslahi yao au kwa ajili ya kuzikiingia kifua tawala kandamizi, vibaraka na tegemezi kama Israel na Saudi Arabia. 
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana