Featured

    Featured Posts

AJALI YA TRENI YA UOKOAJI NA KIBERENGE YASABABISHA VIFO VYA WATUMISHI WATANO WA TRC

Na Mwandishi Maalum, TRC
Watumishi watano wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) wamefariki dunia kufuatia  ajali ya Treni ya Uokoaji kugongana na Kiberenge No.HDT-3 katika maeneo yaliyopo kati ya stesheni za Mwakinyumbi na Gendagenda, eneo liliilopo katika Reli inayotoka Ruvu Junction  mpaka Mruanzi Junction, jana, Machi 22, 2020.

Taarifa ya TRC imewataja waliokufa kuwa ni Ramadhani Gumbo wa DTM Tanga, Injinia Fabiola Moshi wa DME Dar es Salaam, Joseph Komba wa ATM Dar es Salaam, Philip Kajuna -Safety Technical na George Urio - Dereva wa trolley

"Watumishi wa TRC walikuwa sita, Watumishi wanne wamefariki pale pale  katika eneo la ajali na majeruhi wawili walifikishwa katika Hospitali  ya  Magunga ya Wilaya ya Korogwe kwa huduma za Kitabibu.

Mpaka  ilipofikia saa 5 usiku Mach 22, 2020 majeruhi mmoja alifariki na kufikia jumla ya  watumishi watano waliofariki", imesema taarifa hiyo ya TRC

Taarifa hiyo imesema hadi sasa majeruhi mmoja aliyabaki Elizabeth Bona ambaye in Guard was treni  anaendelea na matibabu katika hospitali  hiyo.

"Aidha uchunguzi wa kujumuisha taasisi zingine utafanywa kubaini chanzo cha ajali hii hiyo", imesema taarifa hiyo.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana