Featured

    Featured Posts

SPIKA NDUGAI ASIMAMISHA ZIARA YA KAMATI ZA BUNGE KUEPUKA CORONA, AZIRUDISHA DODOMA

Spika wa Bunge Job Ndugai, akizungumza na Waandishi wa Habari, Ofisini kwake jijini Dodoma leo.

DODOMA, Tanzania
Spika wa Bunge Job Ndugai ameziagiza kamati zote za Bunge za kisekta kusitisha ziara zao akizitaka Kamati hizo ambazo tayari zipo kwenye mikoa mbalimbali nchini zikikagua miradi kusitisha ziara hizo na kurejea jijini Dodoma mara moja.

Akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma leo, Spika Ndugai amesema kwa kipindi hiki Kamati zitafanyika katika maeneo ya Bunge kwa zamu mchana na jioni ili kuzuia msongamano wa watu kama ilivyoelekezwa na Wizara ya Afya.

" Ninaziagiza kamati kurejea Dodoma na shughuli zote zitafanyika hapa bungeni, tayari tushachukua hatua za kuweka vitakasa mikono na vipima joto kwenye magari ya bunge lengo likiwa ni kuchukua tahadhari kuepuka maambukizi.

Pia kwa sasa pia tumechukua uamuzi wa kuzuia watu mbalimbali au vikundi ambavyo vimekua vikija kutembelea bunge kwa ajili ya kujionea shughuli zake," Amesema Ndugai.

Kuhusu ufanyaji wa kazi kwa sasa, Ndugai amesema shughuli nyingi za kuchambua bajeti kwa sasa zitafanyika kwa njia ya mtandao kwa kuwa kuna mtandao wa Bunge.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana