Featured

    Featured Posts

WATU 27 WALIOCHUKULIWA SAMPULI VIRUSI VYA CORONA WAPO SALAMA

Watu 27 waliochukuliwa sampuli ya vipimo vya Corona Tanzania, wako salama
Watu 27 ambao waliliochukuliwa sampuli za vipimo vyao vya afya ili kuwachunguza iwapo wameambukizwa virusi vya Corona Covid-19, wapo salama.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha ufuatiliaji wa magonjwa ya mlipuko katika Wizara ya Afya, Dk Janeth Mghamba akiwa na mtaalam wa majanga wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk Faraja Msemwa. Wakizungumza na waandishi wa habari mjini Arusha, maafisa hao wa Wizara ya Afya nchini Tanzania, wamesema watu hao 27 walichukuliwa sampuli baada ya kubainika kuwa walikutana na dereva wa teksi ambaye alimbeba mgonjwa wa Corona, hivi karibuni. "Watu hawa walikuwa karibu na dereva na baada ya kuchukuliwa vipimo na kupelekwa maabara kuu iliyopo jijini Dar es Salaam wamebainika hawajaambukizwa." Amesema Dk Mghamba. Pamoja na hayo amesema kuwa watu hao, wataendelea kufuatiliwa hadi vitakapofanyika vipimo vya mara tatu kama ambavyo Shirika la Afya Duniani WHO imeagiza.


Janeth Mghamba, Faraja Msemwa wa WHO na Mkuu wa Mkowa wa Arusha
Kwa upande wake Dk Faraja Msemwa amesema kuwa, hadi sasa mkoa wa Arusha hauna mgonjwa mwingine wa Corona zaidi ya Isabella Mwampamba ambaye hali yake inaendelea kuboreka. Naye Mrisho Gambo, Mkuu wa Mkoa Arusha, amewataka wakazi wa mkoa huo kuondoa hofu ya ugonjwa huo, na badala yake waendelee kuchukua tahadhari. Wakati huo huo, Bunge la Tanzania limesitisha utaratibu wa kupokea wageni mbalimbali wakiwamo wanafunzi wanaokwenda bungeni kwa lengo la kuona na kujifunza shughuli za Bunge hilo. Katika taarifa iliyotolewa leo na kitengo cha mawasiliano na uhusiano wa kimataifa cha ofisi ya Bunge, imesema kuwa hatua hiyo ni katika mikakati ya muhimili huo uliotangazwa na Spika Job Ndugai wa kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona. Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa, wageni watakaoruhusiwa kuingia bungeni ni wale wenye kazi na vibali maalum tu.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana