Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kata ya Makongo, katika jimbo la Kawe, Dar es Salaam, Janeth Mahawanga akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza kina mama wa CCM walionyakuwa viti vyote katika Kata hiyo wakati nwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, uliofanyika mwaka jana. Kulia ni Mgeni rasmi, Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, Grace Haule na kulia ni Katibu wa UWT Wilaya ya Temeke Huba Issa. PICHA ZAIDI>> BOFYA HAPA
MAKONGO, Dar es Salaam
Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Kata ya Makongo iliyopo katika Jimbo la Kawe jijini Dar es Salaam, umefanya sherehe ya kuwapongeza kina mama 13 wa CCM ambao wazoa viti vyote katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika mwaka jana na kukiwezesha Chama Cha Mapinduzi kutwaa mitaa yote minne iliyopo katika Kata hiyo.
Katibu wa UWT Kata ya Makongo Juu, Deodath Komba aliitaja mitaa hiyo iliyonyakuliwa yote na kina mama wa Chama Cha Mapinduzi kuwa ni Makongo, Mlalakuwa na Mbuyuni ambako kila mtaa walishinda watatu, huku mtaa wa Changanyikeni wakishinda wanne.
Katika sherehe hiyo iliyofanyika jana na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo mwanasiasa wa siku nyingi na mwanaharakati wa haki za wanawake Getrude Mangela ambaye ni mlezi wa UWT Kata ya Makongo, Mgeni rasmi alikuwa Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, Grace Haule.
Pamoja na kuwapongeza, UWT Kata ya Makongo imewataka kina mama hao walishinda kuwa mabalozi wachapa kazi , Watendaji wazuri, wafuatiliaji wa kero na kuwa wepesi kutoka huduam stahiki kwa jamii ili kila mmoja aone na kuthibisha kuwa wanawake wanaweza.
" Tunawaomba wakawe wabunifu kwenye kazi zao katika kutatua kero na kuhakikisha mabadiliko makubwa ya kiutendaji yanafanyika kwenye mitaa yetu ili hata ufikapo tena wakati wa uchaguzi kina mama tuweze kuchukua nafasi zote na miataa kwani inawezekana na hata kina baba, Vijana na jamii yote kwa ujumla ione hakuna sababu ya kuwa na mashaka kumpa nafasi mama kuongoza jamii", alisema Katibu katika risala hiyo.
Akieleza changamoto alisema miundombinu ya Kata hiyo ya Makongo hasa suala la barabara limekuwa kero ya mda mrefu isiyotatuliwa kwa mda miaka yote kiasi kwamba imesababisha wananchi kukata tamaa kabisa na pia kuomba mtaa wa Makongo ugawanywe ili wapiga kura wasipate kwenda kupiga kura kwa maelezo kwamba mtaa huo ni mkubwa hivyo Wasiojiweza wakiwemo wazee huhindwa kufika maeneo ya kupigia kura.
Post a Comment