Featured

    Featured Posts

KANISA HALISI LA MUNGU BABA TEGETA LAFANYA IBADA MAALUM KUITIKA MWITO WA RAIS DK. MAGUFULI KUHUSU CORONA

Kiongozi wa Kanisa Halisi la Mungu Baba, Baba wa Uzao, akiomba huku akiwa amelala sakafuni, wakati wa Ibada Maalum  ya Kumuomba Mungu Baba, ugonjwa wa Corona usiingine Tanzania, Ibada hiyo ikiwa ni kutitikia mwito wa  Rais Dk. John Magufuli wa kuwataka waumini wa dini mbalimbali wakiwemo wa makanisa na misikiti kumuomba Mungu ugonjwa huo usiingie hapa nchini.  KWA PICHA NYINGINE NYINGI, TAFADHALI >> BOFYA HAPA



TEGETE, Dar es Salaam
Kanisa Halisi  la Mungu leo limetumia ibada yake ya Jumapili, kufanya ibada maalum ya kumuomba Mungu Baba, ugonjwa wa Corona usiingie Tanzania, ibada hiyo ikiwa ni kuitikia mwito wa Rais Dk. John Magufuli alioutoa hivi karibuni, akiwataka waumini wa dini mbalimbali wakiwemo wa Makanisa na Misikiti kumuomba Mungu ugonjwa huo usiingie hapa nchini.

Ibada hiyo ambayo pia ilihusisha maombi ya kuufuta ugonjwa huo katika nchi ambako umeshaingia, imefanyika katika Kanisa Halisi la Mungu Baba, lililopo Tegeta nje kidogo ya Jijini la Dar es Salaam, ikiongozwa na Kiongozi wa Kanisa hilo ambaye Kanisa hilo linamtambua kwa jina la Baba wa Uzao.

"Katika kitabu xha Yona 3:6-9 Mfalme wa Niwawi alipopata habari baada ya siku 40 Taifa litaangamia, alitoa mwito au kuagiza watu wote na mifugo na wanyama wa niwawi wafunge na kuvaa nguo nza magunia ili Mungu  Baba awahurumie na kuingilia kati tatizo lililokuwa mbele yao!

Juzi 10, Kiselu, 1(13 Machi, 2020) Mheshimiwa Rais alitoa mwito kwa viongozi wa Kanisa kuombea Taifa ili ugonjwa mbaya wa Corona (ambao haujaingia Tanzania), usiingie na wale waliokwishavamiwa na ugonjwa huo ufutike ili ujenzi wa uchumi uendelee", alisema Kiongozi wa Kanisa hilo Baba wa Uzao na kuongeza;

"Kitabu kinasema kuwa, viongozi watendao haki, wanawekwa madarakani na Mungu Baba (Rumi 13:1-2) Kiongozi wa Kanisa Halisi hawezi kupuuzia mwito uliotolewa na Kiongozi wa Taifa maana Ninawi, kama tulivyosoma pale katika Yona 3:6-9) walisikiliza mwito wa Mfalme wao, walipotubu wakapona.

Hivyo mimi na uzao wote wa Mungu Baba tumeitikia mwito nhuu na kufanya Ibada Maalum kwa sababu zifuatazo; Mheshimiwa Rais anaishi Moyo wake maana yake ni kiwamba yeye ni Haki ya Mungu Baba. Katika Kitabu cha Mithali 14: 34(a) kitabu kinasema Haki inainua Taifa; hivyo huwezi kupuuza  mwito wa haki ya Mungu Baba.

Uchumi wa wa Taifa umeinuka kwa mda mfupi , sisi wote ni mashahidi ; lazima tuuinue uchumi huu kwa ibada  maalum ili uharibifu uliokuwa umekusudiwa na waovu kudidimiza uchumi wa taifa , usitokee".

Mkuu wa Kanisa hilo alisema, sababu nyingine ni kwamba; "Rais Dk. John Magufuli anajali masikini (wanyonge) . Maana yake ana tabia ya kujali maslahi ya wale wasio nna uwezo wa kujitetea wao wenyewe. katika Mithali 19:17 Kitabu kinasema kuwa ukimsaidia masikini (mnyonge) umemkopesha Mungu Baba naye atakulipa. Mwito aliotoa ni wa kujali masikini", alisema Kiongozi wa KIanisa hilo.

"Huwezi kupuuza kiongozi Kiama Rais Dk. Magufuli ambaye anahurumiwa masikini au wanyonge maana huyo anamkopeshya Mungu Baba na analipwa kila siku. Kwa mantiki hiyo mwito ule wa Rais unahusu wasio na uwezo wa kujitetea wenyewe lazima tuuitikie kwa ibada ili itokee kama mwito ulivyosema", alisema Kiongozi huo.

Katika Ibada hiyo maalum ambayo ilihudhuriwa na maelfu ya waumini baada ya kufafanua kwa nini Kanisa hilo limeitikia mwito wa Rais Dk. Magufuli na kufanya ibada hiyo Maalum, kiongozi nhuyo aliyoa shuhuda mbalimbali kuhusu mafanikio yaletwayo na  ibada maalum na baadaye kufanya maombi katika ibada hiyo Maalum.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana