Featured

    Featured Posts

BOSI WA AMAZON AZOA BILIONI 24 KUTOKANA NA MLIPUKO WA CORONA

Amazon founder and chief executive Jeff Bezos

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Mwanzilishi wa kampuni ya Amazon ameshuhudia utajiri wake ukichupa kwa kiasi cha dola bilioni 24 (sawa na pauni bilioni 19) kutokana na uhitaji mkubwa wa manunuzi kwa njia ya mtandao.
Jeff Bezos sasa ana utajiri wa dola bilioni 138, kwa mujibu wa orodha ya mabilionea inayojumuisha na jarida maarufu la biashara la Bloomberg, akisalia katika nafasi yake kuwa ni mtu tajiri zaidi duniani.
Amazon imepata faida zaidi kutokana na manunuzi yaliyofanywa na watu ambao wamelazimika kukaa nyumbani kutokana na mlipuko wa janga la virusi vya corona.
Kampuni hiyo imekuwa ikiajiri maelfu ya wafanyakazi ili kuendana na kasi ya mahitaji ya wateja.
Hata hivyo, Amazon imekuwa ikikosolewa na wafanyakazi nchini Marekani kuhusu usalama wao mahali pa kazi wakati huu wa mlipuko wa virusi.
amazonHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAmazon ni kampuni kubwa zaidi ya kuuza na kusambaza vifurushi mtandaoni.
Bwana Bezos anamiliki 11% ya hisa katika kampuni ya Amazon na Jumanne ya wiki iliyopita, hisa zilipanda kwa 5.3%.
Familia inayomiliki maduka makubwa ya rejareja ya Wal-Mart, ambao pia wanamiliki kampuni ya Asda inayofanya biashara kwa njia ya mtandao nchini Uingereza nao pia wamepata faida kubwa wakati huu wa mlipuko wa virusi vya corona.
Wanafamilia hiyo ya Walton wametajwa kuwa familia tajiri zaidi duniani baada ya utajiri wao kupanda kwa 5% mwaka huu na kufikia dola bilioni 169, kwa mujibu wa Bloomberg.
Coronavirus
Banner
Kutokana na mamilioni ya watu duniani sasa kufanyia kazi nyumbani, mikutano ya Zoom imefanya utajiri wa mmiliki wake Eric Yuan kupanda mara mbili zaidi na kufikia dola bilioni 7.4.
Bloomberg imesema matajiri 500 duniani wamepoteza kiasi cha dola bilioni 553 kwa mwaka huu mpaka hivi sasa.
Wawekezaji kwenye soko la dunia la mafuta na gesi wameshuhudia kuanguka kwa gharama za mafuta ghafi kutokana na kushuka kwa mahitaji.

Kupanda kwa umaarufu wake

Bwana Bezos alianzisha kampuni ya Amazon mwaka 1995 kwa thamani ya dola 100,000 fedha zake na za familia. Aliacha kazi yake ya awali katika mfuko wa uwekezaji akiwa na miaka 30 baada ya kugundua kuwa kuna ukuaji mkubwa wa matumizi ya mtandao.
Aliungana na mke wake MacKenzie,ambaye walikutana wakati wote walipokuwa wakifanya kazi kwenye shirika la mfuko wa uwekezaji New York , DE Shaw. Wana watoto wanne.
Wenza hao waliachana mwaka 2019, kutengana kwao ambako kuliripotiwa kwa kiasi kikubwa na vyombo vya habari vya kibiashara.
Kama sehemu ya talaka Bi MacKenzie alipata dola bilioni 38 na umiliki wa 4% ya hisa katika kampuni ya Amazon.
Jeff Bezos na aliyekuwa mkewe Bi MacKenzieHaki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionJeff Bezos aliachana na mkewe Bi MacKenzie mwaka 2019
Ndani ya mwezi mmoja wa kuanzishwa kwake, tayari ilikuwa na wahitaji katika majimbo yote 50 na nchi 45 kwa mujibu wa mwandishi wa jarida la maelezo kumhusu bilionea huyo lililoandikwa na Brad Stone mwaka 2013.
Katika kipindi cha miaka mitano ya kwanza Amazon ilipata faida kutoka dola 511,000 mpaka zaidi ya dola bilioni 1.6.
Wawekezaji wakubwa walijitokeza kuwekeza kwenye Kampuni kutokana na mafanikio hayo ya biashara kwa mtandao.
Mwaka 1997, kampuni hiyo iliingia katika soko la hisa na kuzoa dola milioni 54 na kumfanya Bezos kuwa moja ya watu matajiri kabla hata ya kufikisha miaka 35.
Mwaka 1999, jarida la Time Magazine lilimuorodhesha kama moja ya watu maarufu vijana zaidi wa mwaka, na kumuita "mfalme wa biashara ya mtandaoni".
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana