Katika kuunga mkono mapambano dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Dk Ombeni Msuya amekabidhi mashine za kunawa wilayani Mwanga Mkoani Kilimanjaro.
Dk Msuya amekabidhi mashine mbili katika Zahanati ya Mamba iliyopo Ugweno Mwanga pamoja na Mashine zingine mbili katika soko la Kikweni lililopo ndani ya Tarafa hiyo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Dk Msuya amewataka wananchi hao wa Mwanga kuendelea kuchukua tahadhari kama ambavyo serikali na watalaamu wake wamekua wakishauri ili kuweka kujikinga na Ugonjwa huo.
" Niwaombe ndugu zangu mzidi kuchukua hatua kwa kuvaa barakoa, kunawa mikono yenu kwa maji yanayotiririka pamoja na sabuni lakini pia kuwahi hospitalini mara tu unapohisi dalili za ugonjwa huu.
Ni jukumu letu sote sisi kama wananchi kushirikiana na serikali yetu katika kutoa elimu ya kujikinga na ugonjwa huu lakini pia kusaidia vifaa kama hivi ili kuweza kusaidia kujikinga na ugonjwa wa Corona, " Amesema Dk Msuya.
Post a Comment