Featured

    Featured Posts

RAIS DK. MAGUFULI AENDA KUTOA POLE NYUMBANI KWA MAREHEMU BALOZI JOB LUSINDE JIJINI DODOMA, LEO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mke wa Marehemu Balozi Job Lusinde, Mama Sara Lusinde aliyekaa katikati mwenye kilemba cheupe baada ya kuwasili kwa ajili ya kutoa pole nyumbani kwa Marehemu Balozi Lusinde Uzunguni jijini Dodoma, leo.
....................................
Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 09 Julai, 2020 amekwenda kutoa pole kwa familia ya Balozi Mstaafu Job Lusinde aliyefariki dunia tarehe 07 Julai, 2020.

Msiba wa Balozi Mstaafu Lusinde upo nyumbani kwake Kilimani Jijini Dodoma.

Mhe. Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amekwenda nyumbani hapo akitokea Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma ambako ameongoza Kikao cha Kamati ya Maadili na Usalama na Kikao cha Kamati Kuu ya CCM.

Akiwa nyumbani kwa Marehemu Balozi Mstaafu Lusinde, Mhe. Rais Magufuli amekutana na Mjane wa Marehemu Bi. Sara Lusinde, ndugu, jamaa na marafiki wa Marehemu ambapo ameeleza kuwa kuguswa na kifo cha Balozi Mstaafu Lusinde na kwamba daima atamkumbuka kwa mchango wake alioutoa akiwa Waziri wa Ujenzi, ushauri wake mzuri na moyo wake wa upendo na ukweli.

Mhe. Rais Magufuli ameeleza kuwa wakati wa utumishi wake Balozi Mstaafu Lusinde alikuwa mzalendo wa kweli, mchapakazi na aliyetetea maslahi ya Tanzania nchi ya nchi, na kwamba hata alipostaafu aliisemea vizuri Dodoma.

Amewataka wafiwa wote kuwa wastahimilivu na kumpuzisha salama hapo kesho tarehe 10 Julai, 2020 atakapozikwa.



author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana