Featured

    Featured Posts

DK KABATI: WANAWAKE TUTAKIMBIA MCHAKA MCHAKA KILA JIMBO KUZISAKA KURA ZA DK MAGUFULI


 MBUNGE Mteule wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Ritta Kabati amesema Wanawake wa Mkoa huo watakimbia mchaka mchaka kila jimbo kuzisaka kura Mgombea Urais wa CCM, Dk. John Magufuli, wabunge na madiwani wa chama hicho.

Dk Kabati ambaye  kipindi kilichopita alikuwa Mbunge wa Viti Maalumu, aliyasema hayo hivi karibuni wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho katika Jimbo la Mufindi Kusini.

Mbunge huyo mpenda maendeleo kiasi cha waliokuwa wabunge wenzie, walimchagua kuwa Mwenyekiti wa wabunge wa mkoa huo, alisema wana kila haki ya kuipigia kura CCM, kwani maendeleo ya wazi yaliyoletwa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk John Magufuli, yanaonekana.

Ili nisimalize uhondo msikilize Dk. Kabati anavyopiga kampeni kwa staili ya aina yake.


author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana