Jeshi la Polisi Mkoani Njombe linawashikilia watu 4 wakiwemo makada watatu wa CHADEMA kwa tuhuma za mauaji ya Emmanuel Mlelwa, Mwenyekiti wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (UVCCM) Iringa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamis Issa amesema Tadei Mwanyika, Mgombea Udiwani Kata ya Utalingolo alikiri kuwa na marehemu na simu ilionesha alikuwa mtu wa mwisho kuongea naye, gari la George Sanga, Mgombea Udiwani (CHADEMA) ndilo lilitumika kuwabeba watu hao na marehemu.
Mtuhumiwa mwingine ni Optatus Mkwera, Katibu Mwenezi wa CHADEMA ambaye kwa mujibu wa maelezo yake ameonekana kushiriki mauaji na mwingine ni Goodluck Mfuse anayejishughulisha na udalali wa magari.
Mwili wa Emmanuel ulikutwa eneo la Bwawa la Maji Kibena na alipotea tangu Septemba 20, aidha, gari la George Sanga Mwanyika lilikutwa na mkanda wa kiunoni wa marehemu.
Post a Comment